Ads (728x90)

NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKISISITIZA JAMBO WAKATI WAUZINDUZI WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KWENYE VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE  JIJINI MBEYA MAPEMA LEO ASUBUHI
BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WALIOJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MPANGO MPYA WA USAJILI WA UZAZI NA VIFO KATIKA MKAKATI WA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO


NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA AKINAMAMA WATANO WENYE WATOTO WALIOCHINI YA MIAKA MITANO WALIOSAJILIWA KATIKA MKAKATI WA USAJILI KWA WATOTO WALIOCHINI YA MIAKA MITANONAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ANGELA KAIRUKI AKIWASILI KATIKA VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE LEO KWA AJILI YA UZINDUZI  WA MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KUPITIA MKAKATI WA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO WALIOCHINI YA MIAKA MITANO, WENGINE KATIKA PICHA NI PAMOJA NA MTENDAJI MKUU WA RITA PHILIP SALIBOKO, MKUU WA WILAYA YA MBEYA DKT. NOURMAN SIGALLA NA MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI YA  RITA VICENT MRISHO

NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAKATI WA UZINDUZI WA MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KUPITIA MKAKATI WA USAJILI KWA WATOTO WALIOCHINI YA MIAKA MITANO KATIKA VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE JIJINI MBEYA

WATOTO KAMA HAWA WANAHITAJI KUSAJILIWA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA ILI KUWAJENGEA MFUMO MZURI WA MAISHA YAO  SIKU ZA USONI


NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKIZINDUA RASMI MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO JIJINI MBEYA LEO ASUBUHI


ASILIMIA 7.7 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ndio waliosajiliwa na na kupata vyeti vya kuzaliwa kati ya asilimia 14 ya watoto wote waliozaliwa ikiwa ni   asililimia 23 tu ya wananchi wote ambao wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa vizazi kwa watoto waliochini ya miaka mitano, ni kwamba takwimu hizo zimekuwa haziridhishi kwa kutambua umuhimu wa usajili na Utunzaji wa kumbukumbu muhimu za vizazi mwaka 2011.

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili kwa watoto waliochini ya miaka mitano kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA)Bw. Vicent Mrisho alisema kudorora kwa mfumo wa usajili kumechangia serikali kukosa takwimu muhimu kwa  mipango ya maendeleo ya Taifa.

Bw. Mrisho alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa takwimu zisizoridhisha za kumbukumbu za vizazi mwaka 2011RITA  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilibuni mkakati wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano wenye lengo la kuboresha hali ya usajili nchini na kuweka kipaumbele kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.

Alisema kuwa kundi hili la watoto chini ya miaka mitano lilichaguliwa kwa sababu ya kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa  anapata cheti kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani na pia kundi ambalo hutumika kama kipimo katika mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za Mtoto na malengo la Milenia.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angela Kairuki ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda alisema mfumo mpya wa usajili ni sehemu ya ugatuaji wa madaraka kupeleka huduma katika ngazi ya serikali za mitaa.

Alisema awali usajili ulikuwa ukifanyika katika ofisi za Mkuu wa wilaya hali ambayo ilichangia kujitokeza kwa idadi ndogo na hivyo kuleta changamoto inayohitaji mipango mahsusi na kwamba mkakati huu utatoa suluhisho kwa mpango wa maendeleo ya Taifa.
Uzinduzi huu wa usajili wa vizazi na vifo utafanyika katika mikoa mitano ya Mbeya, Mwanza,Simiyu, Shinyanga  na Geita  ambapo kwa mkoa wa Mbeya kutakuwa na vituo 333 vya usajili katika ngazi ya ofisi za watendaji wa kata na vituo vya afya.

Post a Comment