Ads (728x90)















TIMU ya Kimondo ya Mbozi Mbeya leo imejihakikishia matumaini ya kucheza ligi daraja la kwanza baada ya kuichapa timu ya Stendi ya Shinyanga Bao 1-0, bao ambalo lilipatikana kwa njia ya penalt dakika ya 20.
Bao hilo lilifungwa na mchezaji Jofrey Mlawa baada ya mchezaji wa timu ya stendi Nelson Mtambo kufanyiwa madhambi karibu na goli la timu ya Stendi Shinyanga, goli lililodumu hadi mpira unamalizika.
Mchezo huo ambao ulikuwa ukichezeshwa na refarii Zayumba Mapunda uligubikwa na rafu za hapa na pale hali iliyomfanya refarii kumzawadia kadi nyekundu mchezaji wa timu ya  Stendi  David Mwita ambaye alimchezea mchezo usio wa kiungwana mchezaji wa timu ya Kimondo.
Aidha timu ya Stendi ya Shinyanga imedaiwa kuwachezesha wachezaji wawili mamluki kutoka timu ya Njombe mji ambao ni John Milenge ambaye katika timu ya Njombe alikuwa akitumia jina la John  Ganga na Tola Mwangonela.
Mchezo huo kumtafuta mshindi wa kwanza na wa pili ambaye ataungana na timu za ligi daraja la kwanza katika msimu ujao,timu hizo zinatarajia kukutana tena huko mjini Shinyanga katika mechi ya marudiano, mchezo mwingine unazikutanisha timu za Polisi Jamii ya Bunda na Friends Rangers ya Jijini Dar.

Post a Comment