Ads (728x90)


MWANAFUNZI ALIYEJILIPUA NA KUFA KWA MADAI YA WIVU WA MAPENZI DODOMA
Taliki Juma (22) aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) - Dodoma, amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Aidha, katika tukio hilo watu wengine wanane waliokuwa karibu na eneo la tukio walijeruhiwa vibaya.

Kulingana na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye eneo la tukio ni kuwa Juma alimwaga mafuta ya petroli kiasi cha lita tano ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali ni kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Irene, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili.(kwa hisani ya dar24.com)

Post a Comment