Ads (728x90)

Watoto hawa wenye umri wa kuwa darasani muda huu wakifanya kibarua cha kubeba tofari kwa ujira wa sh.500 kama walivyonaswa na kamera yetu eneo la Sinde Jijini Mbeya,watoto hawa walikuwa wakihamisha tofari hizo kuelekea katika eneo la ujenzi,ajira kwa watoto limekuwa ni tatizo ambalo linapigwa vita na jamii kutokana na kuwakosesha masomo watoto wenye umri unaopaswa kuwa shuleni.
Usingizi ni starehe, usingizi ni raha, unapokukuta unaweza kulala wakati wowote mahala popote bila kujali lolote, jamaa huyu baada ya kuzidiwa na usingizi kutokana na swaumu kali alilazimika kuegesha gari pembeni ili ajipumzishe kidogo kuepuka ksababisha ajali wakati anaendesha kama alivyokutwa na kamera yetu mtaa wa Uhindini Jijini Mbeya leo mchana.

Post a Comment