Ads (728x90)

Dkt.Sengondo Edmund Mvungi enzi za uhai wake

Dkt. Mvungi akipelekwa katika chumba cha uangalizi maalum ICU kabla hajahamishiwa katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilali pamoja na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi walipotembelea Dkt. Mvungikatika hospitali ya Muhimbili alikolazwa chini ya uangalizi maalum kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini.


Taarifa zilizotujia jioni ya leo zinadai kuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mhadhiri mwandamizi wa sheria Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dkt. Sengondo Edmund Mvungi amefariki leo katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini.

Dkt.Mvungi ambaye pia aliwahi kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi mwaka 2005 alivamiwa na kupigwa mapanga na majambazi ambapo baadaye alilazwa katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu (ICU)kabla ya kuhamishiwa nchini Afrika Kusini Novemba 7. 

Aidha Jeshi la Polisi kanda maalum limedai kukamata watuhumiwa 9 wanaodaiwa kukutwa na mapanga yanayodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Post a Comment