Ads (728x90)

Ule msemo wa kufa kufaana umejiri leo katika mji mdogo wa Mbalizi ambapo gari la kampuni ya vinywaji baridi vya Pepsi lilipoangusha chupa za soda kwa bahati mbaya na kulifanya kundi kubwa la vijana kuvamia eneo hilo kwa nia ya kutaka kuokota chupa hizo zenye vinywaji ambazo zilikuwa zimevunjika.
Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza wakati gari hilo lilipoingia katika eneo la Stendi ya mabasi Mbalizi ghafla chupa kadhaa za soda zikadondoka chini na kuvunjika ambapo kundi kubwa la vibaka bila kujali kwamba soda hizo zimechanganyika na chupachupa zilizovunjika zungeweza kuwadhuru.
Hata hivyo kijana mmoja mfanyakazi katika gari hilo la vinywaji vya Pepsi alishuka mkuku!!! na kuwatoa baruu vijana waliokuwa wanaokota chupa hizo za soda
Vijana wakiwa wamezunguka chupa za soda mara baada ya masanduku ya soda kuanguka kutoka katika gari

Masanduku ya soda mara baada ya kuanguka kutoka katika gari

Jamaa akiokota baadhi ya chupa za soda baada ya masanduku kudondoka na kuvunja chupa zenye soda

Jamaa wakitoa udenda kwa ajili ya soda zilizoanguka kutoka kwenye gari la Pepsi.

Jamaa akiokoa baadhi ya chupa zilizopona baada ya masanduku kudondoka.

Baadhi ya vijana wakiangalia chupa zilizovunjika na kumwaga soda.
.

Post a Comment