Ads (728x90)

Mlinda mlango wa Mbeya City David Burhani akiwapanga wachezaji wa timu yake wakati wa msukosuko langoni mwa timu hiyo katika mchezo kati ya Mbeya City na Ashanti United, uwnaja wa Sokoine Mbeya City ilishinda kwa goli 1-0

Eneo la jukwaa la wapenzi wa Ashanti lilivyokuwa wakati wa mechi kati ya timu ya Ashanti na Mbeya City.

Golikipa wa Mbeya City David Buruhani akiranda randa katika lango la timu yake

Patashika uwanjani



Golikipa wa timu ya Ashanti Amani Simba akiwa ameudaka mpira huku mchezaji wa timu ya Mbeya City Steven Mazanda akimkaribia

Mcheazaji wa timu ya Mbeya City Paul Nonga akitoka uwanjani baada ya kuumiaa goti nafasi yake ilichukuliwa na mchezaji Yohana Morris.

Golikipa wa Ashanti Amani Simba akiuweka mpira kwa ajili ya kuupiga mbele.


Wachezaji wa timu Mbeya City wakiwapa mikono wachezaji wa timu ya Ashanti kabla ya kuanza kwa mechi kati ya timu hizo uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Mbeya City ilitoka kifua mbele kwa bao 1-0.


Kikosi cha Timu ya Ashanti kilichochuana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Kikosi cha timu ya Mbeya City kilichochuana na timu ya Ashanti katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Ilikuwa ni hatari ya goli katika lango la Mbeya City golikipa David Burhani alikuwa ametoka golini, mpira ulikuwa unaambaa kuingia katika lango la Mbeya City mchezaji wa Mbeya City Antony Matogolo aliokoa jahazi kwa kuutoa mpira huo nje.

Mchezaji wa Mbeya City Antony Matogolo akiwa katika goli la Mbeya City baada kuokoa goli



Ligi Kuu ya Bara imeendelea leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ambapo wenyeji timu ya Mbeya City imeshinda kwa goli 1-0 lililopatikana kwa mchezaji wa timu ya Ashanti  Samir Rubava kujifunga katika dakika 30 ya mchezo.
Ashanti walioonesha kuutawala vyema mpira tofauti na wenyeji Mbeya City, walifanya mashambulizi mengi katika lango la Mbeya City lakini safu ya mashambulizi iliyoongozwa na wachezaji  Farihi Rashid,Husein Sued na Joseph Mahundi ilionekana kushindwa kuelewana katika umaliziaji.
Dakika ya 18 ya mchezo nusura Ashanti ijipatie bao baada ya golikipa wa timu ya Mbeya City David Burhani kutoka golini huku shuti lililopigwa na mshambuliaji wa Ashanti Joseph Mahundi likiambaa ambaa golini kwa Mbeya City ambapo mchezaji wa timu ya Mbeya City Antony Matogolo alikimbilia mpira huo na kuoondosha ukiwa unakaribia kuvuka mstari wa goli.
Hadi mapumziko Mbeya City ilitoka kifua mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza huku kila upande ukiwa umefanya mabadiliko ambapo Mbeya City walimtoa  Hamad Kibopile na kumuingiza  Richard Peter,Yohana Morriss aliingia badala ya Paul Nonga na Mwagane Yeya aliingia badala ya Francis Casto.
Upande wa  Ashanti Abdul Kumbilwa aliingia badala ya Idd Sailas na Richard Lyangile aliingia badala ya Husein Sued.Mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwa upande wowote wa timu bali mashambulizi yalionekana kuwa sawia kila upande.Hadi filimbi ya kumaliza mchezo inapigwa Mbeya City alitoka kifua mbele kwa goli 1-0.
Mbeya City imeendelea kushikilia usukani wa ligi kwa kufikisha jumla ya Pointi 26 nyuma ya Azam kwa tofauti ya idadi ya magoli. 
Mbeya City iliwakilishwa na wachezaji David Burhani, John Kampambe,Hamad Kipobile/Richard Peter,Degratious Julius,Yusuf Abdallah,Antony Matogolo,Alex Seth,Steven Mazanda,Paul Nonga/Yohana Morris,Francis Casto/Mwagane Yeya na Hassan Mwasapili.
Ashanti United iliwakilishwa na Amani Simba,Antony Vicent,Khan Alex,Tumba Lui,Samir Rubava,Idd Sailas/Abdul Kumbilwa,Farihi Rashid,Mussa Mohamed,Paul Maona,Husein Sued/RichardLyangile na Joseph Mahundi.


Post a Comment