Fundi mitambo Daniel Mwakamala akiwa kazini na mtambo wa kusindilia uwanja |
Mwendesha mtambo Daniel Mwakamala akisindilia Uwanja wa Sokoine wakati wa ukarabati wa uwanja huo ambao ulifungiwa na TFF kutokana na kutokodhi viwango. |
Hatimaye kilio cha Wapenzi wa Soka mkoani Mbeya na mikoa ya jirani kinakaribia kumalizika baada ya kuwepo na matumaini ya kukamilika kwa Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ambao ni miongoni mwa viwanja vinane vilivyofungiwa kutochezeshwa mechi za Ligi kuu kutokana na hali ya uwanja huo kutoridhisha.
Jitihada za serikali ya Mkoa wa Mbeya na wadau wa soka wakiwemo Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya MREFA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) uwanja huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80.
Kwa mujibu wa taarifa za Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala ukarabati wa uwanja huo umefikia zaidi ya sh. milioni 20 ambazo ni msaada wa fedha kutoka serikali ya Mkoa wa Mbeya na baadhi ya wadau wa michezo ndani na nje ya mkoa wa Mbeya.
''Tumekopa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali jumla ya Sh. milioni 13.5 zingine tumechangiwa na wadau na wapenzi wa soka jumla tumetumia sh. milioni 22,326,000/-''alisema Mwanjala.
Aliwataja waliokikopesha Chama Cha Mipra wa Miguu mkoa wa Mbeya MREFA kuwa ni pamoja na Chama Cha Mpira wa Miguu nchini TFF Sh. milioni 5, Halmashauri ya Jiji la Mbeya Sh. Milioni 5, Mnassi Communication Sh.Milioni 1.5, Barus General Interprises Sh.milioni 2, na kufikia jumla ya Sh.milioni 13.5.
Mwanjala alisema kuwa fedha zingine zimetokana na michango ya wadau mbalimbali wa soka na kwamba matarajio uwanja huo utakamilika mapema kwa ajili ya mechi ya mzunguko wa pili itakayoanza Januari 25 ambayo itawakutanisha maafande wawili kati ya Timu mwenyeji Tanzania Prison ya Mbeya na Ruvu JKT ya Pwani.
Post a Comment