Ads (728x90)




KAMATI YA WATU KUMI YA “TANZANIA FILM CRITICS ASSOCIATION”-TFCA
Tanzania Film Critics Association ni mradi ulio chini ya Image Profession wenye kuhusisha kundi la wanachama wa hiyari kwa malengo ya kuleta changamoto za kimaendeleo katika Tasnia ya Filamu ikiwa pamoja na kuchambua,kukosoa,kushauri na kusaidia maswala mazima yahusuyo Filamu na wahusika wa Filamu hapa Tanzania.
Pamoja na kufanya shughuli zake kwa kutumia mitandao ya kijamii ,kundi pia litakuwa na shughuli zitakazofanyika katika mazingira mbali mbali ya kawaida ikiwa pamoja na kuwa na mabaraza yatakayohusisha wataalamu mbalimbali wa Tasnia ya Filamu.
Waliopendekezwa watakaoungana na wajumbe watatu kutoka Image Profession(IP)kuingia katika kamati ya watu kumi itakayosimamia na kuratibu utendaji wa Tanzania Film Critics Association,katika kipindi cha miezi sita mpaka mwaka.
Wafuatao ni wajumbe  saba  na idadi ya mapendekezo waliyoyapata kutoka katika mchakato wa kupendekeza uliofanyika kwenye kundi hili kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
1.   John Kitime                                      (47)
2.   Goddy Semwaiko                     (37)
3.   Bishop Hiluka                         (36)
4.   Apilike Gordon                        (33)
5.   Rashid Faraji                           (31)
6.   Rashid Adam                           (25)
7.   Richard Mloka                         (24)
Mkutano wa kwanza wa wajumbe wakamati utakuwa siku ya Jumamosi ya Tarehe 11.02.2012 ,tunatoa shukrani kwa kila mmoja aliyeshiriki katika mchakato mzima wa kundi na wale wote wanaochukuwa muda wao kutoa mada mbalimbali kuchangia na hata kusoma yale yanayoandikwa kwenye kundi..

Post a Comment