Ads (728x90)

Madaktari wa JWTZ waanza kazi Muhimbili

Dar es salaam

MADAKTARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wameanza kutoa huduma ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kukabiliana na upungufu wa madaktari uliosababishwa na mgomo unaoendelea.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Dar es Salaam , Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Khajji Mponda alisema madaktari hao wameanza kufanya kazi katika Hospitali hiyo kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoyatoa juzi alipozungumza na vyombo vya habari.
"Tumewaomba wenzetu kutoka katika Jeshi letu ili kusaidia kutoa huduma za kitabibu kama Waziri Mkuu alivyoagiza'' alisema Mponda.
Alisema madaktari 15 kutoka Jeshini ndio walioanza kutoa matibabu katika Hospitali hiyo ili kukabiliana na uhaba huo uliotokana na madaktari walioopo kwenye mafunzo kugoma.
Alisema madaktari hao wanafanya kazi katika kitengo cha huduma za dharula kutokana na eneo hilo kudorora kwa huduma na kuzidiwa na wagonjwa.
Alisema huduma za kitabibu zinaendelea kama kawaida kufuatia baadhi waliokuwa kwenye mgomo kuendelea kufanya kazi ingawa baadhi yao hasa wale walioopo kwenye mafunzo kuendelea na mgomo huo.
Alisema madaktari waliorudi kazini wamewasirisha madai yao serikali jambo ambalo ni zuri kuliko njia waliyokuwa wanaitumia ya kugoma.
"Serikali ipo tayari kukutana na madaktari hao hasa hao waliorudi kazini ilikufikia muafaka wa madai yao lakini wale wanao lalamikia vichochoroni haitashughulika nayo'' aliongeza Mponda.
Alisema mbali ya madaktari hao kutoka jeshini wamepata madaktari wengine 80 kupitia programu mbalimbali za Wizara yake na kwamba upungufu utakaojitokeza katika hospitali za mikoani ambazo madaktari wao wapo kwenye mgomo huo ameagiza lishughulikiwe na Ofisi za Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI).
"Kama itatokea kuwa na uhaba wa madaktari katika hospitlai zilizopo mkoani tutawapatia madaktari lakini suala hilo tumewaachia wenzetu kupitia TAMISEMI'' alisema Dk.Mponda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (M0I), Profesa Laurence Miseru alisema wameamua kusitisha huduma za kliniki katika Hospitai hiyo ili kukabiliana na uhaba huo wa madaktari.
"Madaktari hao watafanya kazi katika maeneo muhimu katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa ya Moi na kitengo cha magonjwa ya dharura'' alisema Miseru.
Aliongeza kuwa hivi sasa hali ya matibabu kwenye hospitali hiyo imetengamaa ingawa katika baadhi ya wodi kumekuwa hakuna wagonjwa.
Ametoa wito kwa wananchi kuondoa wasiwasi waliokuwa nao kuwa katika hospitali hiyo hakuna matibabu kwamba wafike kutibia baada ya huduma kuanza kutolewa.

STORI NA PICHA KWA HISANI YA DOTTO MWAIBALE WA JAMBO CONCEPT

Post a Comment