Ads (728x90)


-Wanyimwa chakula cha usiku
 -Walazimishwa kufua nguo za ndani na kuosha vyombo
 
NAIROBI,Kenya
WANAUME katika miji ya mikoa ya Kati na Nairobi nchini Kenya    wamedhamiria kuitisha mgomo wa kula kwa juma zima kwa kile walichosema kupinga kitendo cha Kupigwa na wake zao.







Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanaume nchini Kenya Nderutu Njoka amesema kuwa wanawake hao wamekuwa na tabia ya kuwapiga wanaume na kuwanyanyasa kupita kiasi ikiwemo kuwanyima  ‘chakula cha usiku’ hali inayofanya wakose raha.
‘’Tumeazimia kugoma kula majumbani mwetu kwa juma moja kushinikiza wanawake kuacha vitendo vya kuwapiga wanaume zao..wanawake wanafanya unyanyasaji dhidi ya wanaume,;;anasema Bw. Njoka.
Hata hivyo kwa upande wa wanawake nchini humo wamedai kuwa,wanaaume wengi hususani katika mikoa ya Kati Na Nairobi nchini Kenya wamekuwa  ni sawa na ‘wanaume suruali’wamekuwa wakiishi kwakuwategemea wanawake badala ya kujishughulisha na utafutaji wa riziki.
‘’Wanaume pande za hapa kwetu wamekuwa ni ‘’Wanaume Suruali’ hawako na mbinu za kujua kutafuta chapaa ndio maana wanakutwa na Kipigo cha mara kwa mara’’ alisema mwanamke huyo mkazi wa mkoa wa Kati.
Imedaiwa kuwa takribani wanaume 500,000 wamekuwa wakikumbwa na vipigo kutoka kwa wanawake zao ikiwemo kuwanyima  ‘Chakula cha Usiku’kuwalazimisha kufua nguo za ndani na kuosha vyombo ambapo hata katika kulala hulazimika kulala ‘Mzungu wa Nne’na wanaume wanapohitaji kustarehe na wake zao hupigwa Kipepsi.
(Kwa msaada wa BBC SWAHILI)

Post a Comment