Ads (728x90)

Kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiya nchini Amir Tahir Mahmood Chandry (katikati)akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ukumbi wa Mbeya Hotel leo asubuhi

Kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiya nchini Amir Tahir Mahmood Chaundry akisalimiana na baadhi ya waumini wa Jumuiya hiyo mara alipowasili uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya leo asubuhi






Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiya nchini



JUMUIYA ya Waislamu wa Ahmadiya nchini imesema kuwa sababu za machafuko katika nchi za Mashariki ya Kati ambako asilimia kubwa ni waislamu zimetokana na waislamu kutofuata kwa vitendo muongozo wa Koran Tukufu na Hadithi sahihi za Mtume Muhammad (SAW).

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiya nchini Amir Tahir Mahmood Chaundry mara alipowasili Jijini Mbeya kwa ajili ya ziara ya Mkutano wa Amani inayofanyika Jijini hapa.

Amir Chaundry alisema kuwa mchango wa Uislamu katika amani ya nchi na dunia ni mkubwa na kwamba machafuko yanayoendelea katika nchi nyingi zenye waislamu wengi zinatyyokana na waislamu wenyewe kutofuata maagizo yanayofundishwa katika Kitabu kitukufu cha Koran. 

Akijibu swali kuhusu wajibu wa Jumuiya hiyo katika kusimamia amani duniani ilhali nchi nyingi za kiislamu zina machafuko, Kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika Jumuiya ya Ahmadiya nchini alisema, wajibu wa waislamu ni kutii sheria na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Alibainisha kwa kusema kuwa hali inayotokea katika nchi nyingi ikiwemo nchi aliyotokea ya Afghanistan imetokana na kuwepo kwa waislamu wasiojua vyema uislamu.

Alisema kuwa waislamu wengi wako kwa majina lakini hawatekelezi Uislamu kama unavyoagizwa na Mwenyezi Mungu na kuwa Jumuiya ya Ahmadiya kwa nafasi yake imejitahidi kutangaza amani na utulivu duniani kote kwa njia za midahalo,makongamano ya kidini, mikutano na kusambaza vipeperushi.

Akinukuu baadhi ya aya za Koran Amir Chaundry  alisema kuwa Jumuiya ya Ahmadiya inaamini kuwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu mahala atakako bila kushurutishwa  na mtu yoyote.

''Utaona katika nchi za Kiislamu, Waislamu kwa waislamu wanauana wenyewe kwa wenyewe, hawa ni waislamu lakini hawaujui Uislamu, tukiusoma vyema Uislamu hakuna vurugu inayoweza kutokea,''alisema Amir Chandry.








Post a Comment