Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu madhehebu ya Answar Sunna wakiungana na waislamu wengine duniani katika ibada ya swala ya Idd katika Viwanja vya Kiwanja Ngoma Jijini Mbeya leo asubuhi |
WAUMINI
wa
dini kiislamu madhehebu ya Answar Sunna mkoani Mbeya wameswali swala ya
Idd leo katika Viwanja vya Kiwanja Ngoma na kuwataka Mashekhe kutotumia
lugha za uchochezi
zinazojenga chuki baina ya Waislamu.
Akizungumza
na umati wa waislamu waliojumuika katika ibada hiyo ya kukamilisha kwa mfungo
wa mtukufu wa Ramadhani, imamu aliyeswalisha swala hiyo Shekhe Ibrahimu Bombo
alisema kuwa baadhi ya Mashekhe wakubwa wamekuwa wakitumia vyombo vya habari
kujenga chuki kwa waislamu.
Alisema, swala
la ibada ni wajibu kwa waislamu wote na kwamba yapo mambo ambayo waislamu
wanatofautiana katika kufanya ibada maalumu ambayo hutokana na uelewa na kwamba
jambo hilo halipaswi kuleta mgongano baina ya waislamu.
‘’Wapo mashekhe wa taasisi fulani hujitokeza katika
vyombo vya habari na kuleta kejeli dhidi ya wengine kuhusu uelewa wa mambo,
hakuna mamlaka iliyo juu ya sheria inayopaswa kuwakejeli ama kuwatukana
wengine, jambo hili lisipoangaliwa linaweza kuleta chuki,’’alisema Shekhe
Bombo.
Alisema uislamu unajengwa kwa umoja na mshikamano na
kama yapo mambo ambayo waislamu wanapishana yanapaswa kujadiliwa kulingana na
mafundisho ya dini hiyo badala ya kundi la watu fulani kujiona ni bora zaidi ya
kundi jingine.
‘’Sisi sote
tunafuata mafundisho ya Kitabu cha Koran na Hadithi za Mtume Muhammad (SAW) anayefuata
mafundisho haya kwa dhati hawezi kukurupuka na kukejeli wengine,’’alisisitiza
na kuongeza.
‘’Wanaohoji
kwa nini tunaswali leo, tunasema kuwa sisi tunaswali mwezi wa Kimataifa
ambao dunia nzima wanaswali,wale watakaoswali kesho hakuna anayewazuia na
wala ninyi msiwakejeli ambao leo bado wamefunga na wao hawapaswi kuwakejeli
ninyi ambao leo mnakula mchana,’’alisema.
Kwa upande
wake Shekhe Rajab Nzunda alisema kuwa Waislamu wanapaswa kufuata na kuendeleza mafundisho
ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wengi waliamua kuacha maasi na kujikita
katika ibada.
‘’Mwezi wa
Ramadhani umetufundisha, uchamungu, hatupaswi kurejea tena katika maovu ambayo
yalitakaswa na Mwezi huu,tusirejee tena kufanya madhambi, tuendeleze ibada na
uchamungu tuliodumu nao kwa mwezi mzima,’’alisema Shekhe Nzunda.
Wallahi mtihani mkubwa,Ilobaki kuomba rehema toka kwa mola. Nauliza nini maana ya umoja ikiwa huyo anayehubiri anatangulia kusaliti kwa vitendo na kula iddi kabla ya kutangazwa na viongozi.Sasa hiyo sio uchochezi?
ReplyDeleteIdd hutangazwa kwa kuandama kwa mwezi si kwa kutangazwa na viongozi
ReplyDelete