Chama cha Mpira wa miguu nchini (TFF) kimetaja majina ya kikosi cha
wachezaji 16 kwa ajili ya maboresho ya timu ya Taifa Stars kati ya
wachezaji 34 waliokuwa katika kambi ya wiki tatu mjini Tukuyu wilayani
Rungwe mkoani Mbeya.
Kikosi hicho ambacho kimeelezwa kuwa ni cha maboresho kinatarajia kucheza mechi mbalimbali za kirafiki ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Hotel ya Hill View Jijini Mbeya kocha
msaidizi wa kikosi hicho Salum Mayanga alisema kuwa wachezaji
walioteuliwa ni pamoja na Mlinda mlango Benedict Tinoko(Mara),Walinzi wa
kati Emma Namwondo Simwanda(Temeke)Joram Nason Mgeveje(Iringa).
Aliwataja
walinzi wa pembeni kuwa ni Omar Ally Kindamba(Temeke)Edward Peter
Mayunga(Kaskazini Pemba),Shirazi Abdallah Sozigwa(Ilala) na viungo wa
ulinzi ni Yusuf Suleiman Mlipili(Temeke) na Said Juma Ally(Mjini
Magharibi).
Wengine
ni viungo wa ushambuliaji Abubakar Ally
Mohamed(Kusini Unguja)Hashimu Ramadhan Magona(Shinyanga) ambapo viungo
wa pembeni ni Omar Athuman Nyenje(Mtwara), Chunga Said Zito(Manyara) na
washambuliaji wanne ambao ni Mohamed Seif Said(Kusini Pemba)Ayubu Kassim
Lipati(Ilala) Abdulrahman Othman Ally(Mjini Unguja) na Paul Michael
Bundala(Ilala).
Pia
Kocha Mayanga aliwataja wachezaji wawili wa U-20 watakaojiunga na timu
Serengeti Boys kuwa ni Mbwana Mshindo Mussa kutoka mjini Tanga na Bayaga
Athanas Fabian kutoka mkoani Mbeya.
Hata
hivyo alisema kuwa wachezaji 16 waliobaki wataendelea kuwa chini ya
uangalizi kwa ajili ya kuziba mapengo kwa timu ya Taifa na kwamba
mchakato wa uteuzi wa wachezaji hao ambao ni mpango mpya wa chama cha
Mpira wa miguu nchini TFF kuimarisha kikosi cha timu ya Taifa umefanyika
mara nne ambapo awali jumla ya wachezaji 143 walijitokeza na kuchujwa
hadi kufikia idadi ya wachezaji 16.
Post a Comment