Waamuzi waliochezesha mechi kati ya Mbeya City na Azam wakitolewa uwanjani na askari polisi |
Askari polisi wakiwa wamejipanga kudhibiti vurugu mmara baada ya mechi kati ya Azam na Mbeya City kumalizika |
Meneja wa timu ya Mbeya City Emanuel Kimbe akiwa ameongozana na shabiki wa timu hiyo wakimwaga machozi baada ya timu yao kufungwa Bao 2-1 na Azam |
''Huu ndio mchezo wa Tanzania... hakuna fare kabisa refarii wametufanyia vibaya angalieni wenyewe''ndivyo alivyokuwa akisema Meneja wa Timu ya Mbeya City Emanuel Kimbe |
''Inakuwaje jamani hapa washikaji washashitukia dili tunatokaje humu uwanjani'' |
Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Mwagane Yeya dakika ya 70 |
Mchezaji wa Mbeya City Mwagane Yeya akishangilia bao aliloifungia timu yake dakika ya 70 |
Benchi la wachezaji wa akiba wa Azam |
Magari ya polisi yakilisindikiza Basi la Azam kutoka uwanjani mara baada ya kumalizika kwa mchezo |
Jukwaa la mashabiki wa Azam |
Wachezaji wa Mbeya city wakitoka uwanjani wakati wa mapumziko wakiwa wamelala kwa bao 1-0 |
Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao lao la kusawazisha |
Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga refarii kwa madai ya kuchezesha kwa upendeleo |
Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi akielezea tatizo la mwamuzi akidai kuwa amechezesha kwa upendeleo |
Mmoja wa wapenzin wa Mbeya City akifuta machozi mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa |
Tafrani hiyo ilitokea baada ya Mbeya City kufungwa bao la pili na mchezaji John Boko wa Azam ambapo kabla ya kufunga goli hilo mshika kibendera namba moja Abdallah Uhako kutoka Jijini Arusha alikuwa amenyoosha kibendera kuashiria kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea.
Ofisa habari wa Mbeya City Freddy Jackson naye hakukosa neno akidai kuwa kulikuwepo na tiketi bandia zilizokamatwa katika mechi hiyo |
Msemaji wa kampuni ya Voidacom Salum Mwalimu akielezea hamasa za mchezo huo na mpango wa kampuni hiyo kutangaza zawadi mapema kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo. |
Mara baada ya kuingia kwa goli hilo golikipa wa Mbeya City alikuwa wa kwanza kumfuata refarii wa mchezo huo Lazaro huku akifuatiwa na wachezaji wengine wa Mbeya City hali iliyosababisha mchezo huo usimame kwa takribani dakika 5.
Tafrani hiyo ambayo ilitokea dakika ya 85 ilisababisha mchezaji wa timu ya Mbeya City Paul Nonga kupewa kadi nyekundu na refarii Lazaro kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alitoa lugha ya mbaya kwa mwamuzi.
Aidha mchezo huo ambao katika kipindi cha kwanza ulitawaliwa zaidi na timu ya Azam kiasi cha kucheza nusu uwanja, wachezaji wa Mbeya City walikuwa wakishindwa kulifikia lango la Azam tofauti na ilivyokuwa katika michezo yake mingine iliyopita hali ambayo ilianza kutoa bishara ya ushindi kwa Azam.
Ilikuwa ni dakika ya 44 ya mchezo ambapo mchezaji wa Azam Gaudence Mwaikimba aliwanyanyua mashabiki wa timu yake kwa kuipatia goli la kwanza baada ya piga nikupige katika goli la Mbeya City.
Mbali na kufungwa kwa goli hilo wachezaji wa Mbeya City walikosa nafasi mbili za wazi baada ya washambuliaji wake kushindwa umaliziaji kwa kupiga mipira nje na kumlenga kipa wa Azam Aishi Manula ambaye hakupata misukosuko ya kutosha langoni kwake.
Hadi mapumziko Azam ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo wachezaji wa timu ya Mbeya City walionekana wakiwa na ari kubwa ya kurudisha bao hilo kiasi cha kulishambulia mara kwa mara lango la Azam ambapo katika dakika ya 70 mchezaji mahiri wa Mbeya City Mwagane Yeya aliipatia timu yake bao la kusawazisha kwa tiktaka lililomuacha golikipa Manula kuchupa bila mafanikio.
Wakicheza huku mvua za rasharasha zikiendelea kunyesha na kusababisha wachezaji kuanguka mara kwa mara kutokana na utelezi, Mbeya City walianza kulishambulia lango la Azam tofauti na kipindi cha kwanza ambacho walionekana wakiusindikiza mpira hadi golini na kushindwa kumalizia.
Wakicheza huku mvua za rasharasha zikiendelea kunyesha na kusababisha wachezaji kuanguka mara kwa mara kutokana na utelezi, Mbeya City walianza kulishambulia lango la Azam tofauti na kipindi cha kwanza ambacho walionekana wakiusindikiza mpira hadi golini na kushindwa kumalizia.
Baada ya goli hilo Mbeya City walianza kulishambulia lango la Azam kama nyuki lakini mara kadhaa wachezaji walipokuwa wakikaribia lango filimbi ya mwamuzi ilipulizwa kuashiria kuwa walikuwa wamezidi hali ambayo ilianza kuibua hisia za upendeleo kwa wachezaji wa Mbeya City kuanza kumlalamikia mwamuzi.
Goli la ushindi kwa Azam lilipatikana dakika ya 85 na mfungaji John Boko na kuzua tafrani kutokana na mchezaji
huyo kuonekana kuotea ambapo mwamuzi namba moja Abdallah Uhako
alinyoosha kibendera lakini mwamuzi wa kati alipuliza kipenga cha
kuashiria goli.
Dakika chache baadaye mwamuzi alipuliza kipenga cha kumaliza mpira ambapo mashabiki walivamia uwanja kwa nia ya kutaka kumdhuru refarii lakini kikosi cha kutuliza ghasi FFU walilazimika kuingia uwanjani kumuokoa mwamuzi na kumkimbiza katika chumba hadi saa 1:45 usiku.
Katika hatua nyingine mashabiki na wapenzi wa timu ya Mbeya City walionekana wakimwaga machozi kutokana na mchezo huo huku wakimlalamikia uchezeshaji wa mwamuzi huyo wakidai kuwa amenunuliwa na timu ya Azam ili timu hiyo ifungwe.
Awali kabla ya mchezo huo kulikuwa na minong'ono iliyovuma Jijini Mbeya kuwa timu ya Mbeya City ilipanga kuuza mechi hiyo ili icheze chini ya kiwango kuipa nafasi Azam ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo, hali ambayo ilianza kuwapa hofu mashabiki katika kipindi cha kwanza chya mchezo huo baada ya Mbeya City kucheza chini ya kiwango.
Kwa mchezo huo Azam inaendelea kushikilia usukani wa ligi ikiwa imefikisha jumla ya point 59 na jumla ya michezo 25 ikiendelea kujiwekea rekodi ya kutofungwa katika ligi hiyo tangu msimu msimu uanze,. ilhali Mbeya City ikivunja mwiko wa kutofungwa nyumbani katika jumla ya mechi 25 ilizocheza huku ikiwa imeshapoteza michezo mitatu na akufungwa jumla ya magoli 19 ikibakiwa na pointi 46 nyuma ya Yanga yenye jumla ya Point 55.
MBEYA CITY
David Burhan,Aziz Sibo/Ahmned Kibopile,Hassan Mwasapili,Yusuf Abdallah,Yohana Moris,Antony Matogolo,Said Kipanga,Steven Mazanda,Paulo Nonga,Mwagane Yeya,na Deus Kaseke.
AZAM FC
Aishi Manula,Erasto Nyoni, Daniel Mbaga,Said Morad,Agrey Morris,Kiple Balu,Himid Mao,Salum Abubakar,Gaudence Mwaikimba,John Boko na Kiple Cheche.
Post a Comment