Mwenyekiti wa Shirika la Without Mother Organization Chriss Zacharia akimkabidhi mafuta ya ngozi Katibu wa Chama Cha Maalbino mkoa wa Mbeya William Simwali. |
Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Jamhuri ya Czech Bez mamy
na Club 75 kupitia shirika lao dada la mkoani Mbeya Without Mother
Organization wameamua kutoa misaada kwa watu wenye ulemavu wa ngozi hasa wanafunzi kwa kuwapatia
misaada ya mafuta yanayokinga ngozi zao na mionzi ya jua.
Mwenyekiti wa shirika la without Mother na Mratibu wa Miradi
wa shirika la Bez Mamy Bw Chris Zacharia alisema wameamua kutoa misaada hiyo
ili kuwawezesha watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao wanavaa sare za mikono mifupi na kaptula
kuhudhuria masomo bila kuogopa mionzi ya jua hasa kuanzia mwezi mei hadi oktoba
''Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanashindwa kuhudhuria masomo vizuri wakati wa jua kali
kwa kuwa wanaogopa jua na hivyo kushuka kitaaluma na kukosa haki sawa kielimu
kama watoto wengine na hivyo kutokuwa na fursa za ajira,'' alisema Zacharia.
Mafuta hayo ambayo yanapatika hapa nchini kwa bei kuanzia
shilingi 30,000 hadi 80,000 kwa chupa yanatolewa bure na shirika la without
mother kwa hisani wa watu wa Jamhuri ya Czech kupitia Bez mamy na Club 75
Pamoja na msaada huo kwa albino Without Mother na Bez mamy
pia wanatoa misaada ya ujenzi na ukarabati wa madarasa, vitabu vya kiada na
madawati katika shule ya msingi Galula wilaya ya Chunya, Shule za msingi Kisa
na Ilenge wilaya ya Rungwe, shule za msingi Mahango na Simike wilaya ya Mbarali
pamoja na ujenzi wa kituo cha watoto yatima katika kijiji cha mahango wilaya ya
Mbarali.(STORI NA PICHA KWA HISANI YA SHIRIKA LA WITHOUT MOTHER ORGANIZATION)
Post a Comment