KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI |
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 17.04.2014.
·
MFANYABIASHARA MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU
KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETTER
MWAMBENE (38) MFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA KIENYEJI, MKAZI WA
KALOLENI – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA
KISOGONI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA HUKO KATIKA MTAA WA KALOLENI, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA
MOMBA MNAMO TAREHE 16.04.2014 MAJIRA
YA SAA 20:00 USIKU. WATU HAO KABLA
YA KUFANYA TUKIO HILO WALIMVIZIA MAREHEMU NJIANI KATIKA UCHOCHORO WAKATI
ANARUDI NYUMBANI AKIWA UMBALI WA MITA CHACHE KABLA YA KUFIKA KWAKE NA KUMVAMIA
KISHA KUMSHAMBULIA. AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU BAADA YA KUPEKULIWA KATIKA
MIFUKO YAKE ALIKUTWA NA KIASI CHA FEDHA DOLA ZA KIMAREKANI 1,460.
MSAKO MKALI
UNAFANYWA NA ASKARI WA TUNDUMA – TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE
– ZAMBIA ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA JUU YA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE/WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment