Mmoja wa jamaa waliohudhuria mahakamani akimwaga machozi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA mtaa wa Itiji kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 kwa kujeruhi.
MWENYEKITI wa serikali ya Mtaa wa
Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA) Ezekiel King(52) na
mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7 kutokana na makosa
ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi wa Itiji mjini
humo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa
Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Juliana William
alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia Mwakasinga kwa kumpiga na
kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji
kilichopo mtaa wa Itiji.
Alisema anawatia hatiani washitakiwa hao kutoka na kuwepo
kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu upande utetezi kugongana na hivyo kuridhika na
ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo
wanayo fursa ya kukata rufaa iwapo hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.
Akitoa mifano ya kesi
mbalimbali zinazoshabihiana na kesi hiyo Hakimu Batulaine alisema kuwa makosa
hayo ni kinyume cha kifungu sheria cha
kanuni ya adhabu namba 225 sura ya 6 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hakimu Batulaine alisema kuwa katika maelezo ya shahidi namba
moja Mwakasinga ambaye ndiye mlalamikaji
ni kwamba alijeruhiwa na kuumizwa na
washitakiwa alipoingia katika kilabu cha pombe za kienyeji na kwamba alifanyiwa hivyo baada ya kuingia ndani
ya kilabu hicho na kusukumwana kuanguka nje.
Alisema katika maelezo hayo shahidi namba moja hadi namba
tatu wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi unaofanana lakini maelezo ya mashahidi
wa upande wa utetezi yanajichanganya na hivyo kutoa mashaka juu ya utetezi wao.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mlalamikaji Mwakasinga
alipigwa na kujeruhiwa na washitakiwa na baadaye washitakiwa hao walimchukua na
kumpeleka kituo cha Polisi wakidai kuwa mlalamikaji Mwakasinga alikuwa akifanya
vurugu kilabuni.
Hata hivyo mlalamikaji ambaye alilazwa katika hospitali ya
rufaa wodi namba nne ambayo hulazwa watu wenye ugonjwa wa akili ili kumpima
kama alifanya vurugu kutokana na ugonjwa wa akili alipotoka alifungua mashtaka
ya kupigwa na washitakiwa hao ambao walikamatwa na kufunguliwa kesi ya kudhuru
mwili.
Katika utetezi wake kabla ya kutolewa hukumu Mshitakiwa King
aliomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na watoto sita na kuwa
hakujua kama kitendo cha yeye kama kiongozi wa mtaa kuamka kwenda kwenye tukio kingemtia hatiani.
|
Post a Comment