Ads (728x90)

Zimesalia takribani dakika 60 kwa timu zenye upinzani wa namna yake katika Ligi Kuu ya Vodacom Mbeya City na Azam FC zitakapoingia uwanjani leo kumeibuka uvumi kuwa timu ya Mbeya City imepanga kuuza mechi hiyo kwa nia ya kujipatia kipato ili kuiachia Azam nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mwaka huu.

Uvumi huo umezagaa kila kona ya Jiji la Mbeya hasa ikielezwa kuwa Mbeya City haina nafasi ya kutwaa Ubingwa kwa nafasi iliyonayo na kwamba ili kujenga historia ya ubingwa kuondoka mikononi mwa timu ya Yanga inapaswa iiachie Azam kwa namna yoyote iwayo.

Timu hizo zinaingia uwanjani huku zikiwa na mvuto wa aina yake hasa kutokana na ukweli kuwa matokeo ya leo ndio yatakayombashiri Bingwa wa Kombe hilo mwaka huu.
Azam inaingia uwanjani ikiwa ina akiba ya point 56 huku ikiwa inashikilia usukani wa ligi hiyo mbele ya Yanga ilhali Mbeya City ikiingia uwanjani ikiwa na alama 46.
Mvuto wa mechi ya leo unatokana na ugeni wa timu hizo katika ligi ukilinganisha na timu za Yanga na Simba ambapo hadi sasa katika wakati kiola timu ikiwa imecheza mechi 24 Azam inaendelea kushikilia usukani kwa pointi 56 ikiwa ina jumla ya magoli ya kufunga 48 na kufungwa magoli 14 na kutoa saare mechi 8 huku ikiwa imeshinda jumla ya michezo 16 na haijapoteza mchezo wowote tangu imeanza ligi.
Timu inayofuatia ni Yanga yenye jumla ya point 52 ikiwa ina jumla ya magoli 58 na kufungwa magoli 17 ikiwa imepoteza michezo 2 na kushinda mechi 17 na kutokaa sare michezo 7.

Mbeya City inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya pointi 46 huku ikiwa imepoteza michezo miwili, imeshinda mechi 12,imetoka sare michezo 10, imepoteza michezo 2, ina jumla ya magoli ya kufunga 30 na kufungwa magoli 17.

Katika mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana zilitoka sare ya 3-3 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi hali ambayo inaongeza ari na mvuto wa mchezo wa leo.

Dakika 90 mchezo wa leo ndizo zitakazotabiri nani bingwa wa Ligi Kuu ya vodacom mwaka huu.


 


Post a Comment