Ads (728x90)


KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA DANIEL MTUKA

BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI YA FOREST WAKIWA KATIKA CHUMBA AMBACHO KIMEPACHIKWA JINA LA GUANTANAMO

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI FOREST JIJINI MBEYA WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA GUANTANAMO WAKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA OFISA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA FOREST JIJINI ,MBEYA
















MMOJA WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI FOREST AKIONESHA NAMNA AMBAVYO WALIMU WANATOA ADHABU ILIYOPEWA JINA LA KUIBEBA DUNIA KATIKA CHUMBA KILICHOPACHIKWA JINA LA GUANTANAMO


KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA DANIEL MTUKA AKITOA MAELEZO KWA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) NAMNA AMBAVYO WALAIVYOFANIKIWA KUWANASA WALIMU WALIOKUWA WAKIWALAZIMISHA WANAFUNZI KUTOA RUSHWA YA SH. 500


SEKONDARI YA KATA YADAIWA KUFUNGUA JELA YA GUANTANAMO.

WALIMU wa shule ya sekondari ya Forest iliyopo jijini Mbeya wamedaiwa kufungua jela maalumu iitwayo Guantanamo inayotumika kwa ajili ya kutoa adhabu na kuwatesa wanafunzi wnaoshindwa kutoa hongo ya sh. 500 wanapofanya makosa shuleni hapo.

Imedaiwa kuwa wanafunzi wanapofanya makosa mbalimbali huitwa na walimu na kushinikizwa kutoa kiasi cha sh.500 hadi 1,000, wanaposhindwa kutoa fedha hizo hupelekwa katika chumba cha Guantnamo ambako hupewa adhabu ya kuweka kichwa chini miguu juu.

Adhabu hiyo iliyopewa jina maarufu la 'Kuibeba Dunia' hufanyiwa wanafunzi wanaoshindwa kutoa hongo ya fedha ambapo wale wanaotoa huachiwa huru na kuendelea na masomo.

Mara baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Kikosi cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mbeya kilituma makachero wake shuleni hapo na kukuta namna ambavyo wanafunzi wanavyopewa adhabu ya kijeshi katika chumba cha Guantanamo.

Wakizungumza namna ambavyo wanapewa adhabu hiyo baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa wapo walimu wawili maalumu kwa kutoa adhabu kwa wanafunzi ambao wameshindwa kutoa kiasi cha sh. 500 kwa ajili ya kujikomboa.

Wamesema kuwa walimu hao huwa na orodha ya wanafunzi wanaofanya makosa kwa siku nzima na kuwaita mmoja mmoja na kuweka alama kwa jina la mwanafunzi aliyetoa fedha na kwamba wale ambao wameshindwa kulipa fedha hizo hutakiwa kuingia katika chumba cha adhabu.

Wanafunzi hao wamebainisha kuwa wanaposhindwa kutoa kiasi cha sh. 500 hupelekwa katika jela ambayo imepachikwa jina la Guantanamo na kupewa adhabu mbalimbali ikiwemo kucharazwa bakora.

Kwa upande wake aliyejitambulisha kwa jina la Sebastian Komba anayesoma kidato cha tatu shuleni hapo amesema kuwa adhabu hiyo ameikuta tangu anaingia shuleni hapo na  kwamba mara nyingi wamekuwa wakilalamika kwa uongozi wa serikali ya shule hadi kwa Mkuu wa shule lakini hakuna ufumbuzi unapatikana.

Naye mwanafunzi wa kidato cha kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Amina Moses alisema wamekuwa wakifanyiwa unyama huo kwa muda mrefu, na kwamba yeye binafsi alimweleza mzazi wake ambapo alisema kuwa atafuatilia kujua undani wake.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka amesewataja walimu hao ambao wamekutwa na jumla ya sh.64,000 kuwa ni Faustin Robert na Josephat Mwasote.


Post a Comment