Ads (728x90)


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKIONESHA BUNDUKI AINA YA SMG NA HIRIZI AMBAVYO VINADAIWA KUTUMIWA NA JAMBAZI ALIYEUAWA


HUYU NDIYE JAMBAZI TULIYEKUWA TUKIMSAKA KWA MUDA MREFU.....OVA!!!TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 25. 03. 2013.

WILAYA YA MBEYA- JAMBAZI MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIWA    
                                     NA WENZAKE KWENYE HARAKATI ZA KUTEKA MAGARI  
                                     ENEO LA MLIMA NYOKA.

·         TAREHE 25.03.2013 SAA 04:00HRS ENEO LA MLIMA NYOKA WILAYA YA MBEYA KULIKUWA NA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA POLISI NA MAJAMBAZI WAPATAO WANNE [4]

·         MAJAMBAZI HAO TAYARI WALIKUWA WAMEWEKA MAWE BARABARANI KWA NIA YA KUTEKA MAGARI ILI WAFANYE UPORAJI KATIKA ENEO HILOAMBALO LIMEKUWA NA MATUKIO KADHAA YA WATU KUPORWA MALI ZAO.

·         JESHI LA POLISI BAADA YA KUPATA HABARI ZA KUTEGWA MAWE, ASKARI WALIFIKA KWA WAKATI KWA KUWA POLISIWALIKUWA JIRANI NA ENEO HILO NA KUWEKA MTEGO KWA KUWA MAJAMBAZI HAWAKUWA WAMEONEKANA KWA WAKATI ULE.

·         BAADA YA MUDA MAJAMBAZI WALIPOONA TAA ZA GARI WALIJITOKEZA TAYARI KUSHAMBULIA LAKINI KABLA YA HAPO POLISI WALITOA AMRI YA KUJISALIMISHA KINYUME CHAKE WAKAANZA KUPIGA RISASI OVYO NDIPO MASHAMBULIZI YA POLISI YAKAFANYWA.

·         KATIKA MAPAMBANO ALIJERUHIWA JAMBAZI MMOJA KWA RISASI KIUNONI NA UBAVUNI KULIA ,ALIPOWAHISHWA HOSPITALI KWA MATIBABU DAKTARI ALIBAINI KUWA AMEKWISHA FARIKI.

·         JAMBAZI HUYO ALIKUTWA NA SILAHA MOJA SMG NA AB NA NAMBARI NYINGINE ZIKIWA ZIMEFUTWA NA MAGAZINE YAKE IKIWA NA RISASI ISHIRINI NA MBILI [22] PAMOJA NA MAPANGA MAWILI [2].

·         ALIPOFANYIWA UPEKUZI MAUNGONI MWAKE JAMBAZI HUYO ALIKUTWA NA KITAMBULISHO CHA MKAZI CHENYE NAMBA B.0010453 CHENYE JINA LA EMANUEL BLASIUS MDENDEMI ALIYEZALIWA MWAKA 1984 ENEO LA MATAMBA WILAYANI MAKETE-IRINGA.MAKAZI YAKE NI UWEMBA – NJOMBE.

·         JAMBAZI HUYU AMEBAINIKA KUWA NI MIONGONI MWA MAJAMBAZI WALIOKUWA KWENYE MTANDAO WA MAJAMBAZI ULIOKAMATWA HIVI KARIBUNI KUHUSIANA NA MATUKIO WALIYOFANYA MIKOA MBALIMBALI IKIWEMO MBEYA,NJOMBE NA IRINGA.AIDHA AMEBAINIKA KUSHIRIKI

KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA ASKARI POLISI PC JAFARI WA KITUO CHA MKWAJUNI – CHUNYA TAREHE 06.02.2013.

·         UFUATILIAJI WA MAJAMBAZI WALIOTOROKA UMEENDELEA KUFANYWA.KAMANDA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WAHALIFU HAO AZITOE BILA KUCHELEWA KWA JESHI LA POLISI ILI ZIFANYIWE KAZI.AIDHA KAMANDA ANAENDELEA KUWATAHADHARISHA MAJAMBAZI /WAHALIFU WA MAKOSA YEYOTE KUACHANA NA UHALIFU KWA KUWA NI BIASHARA ISIYOLIPA/ISIYO NA FAIDA BADALA YAKE WAFANYE SHUGHULI HALALI KUPATA MAENDELEO AMBAZO FURSA ZAKE NI NYINGI.

2.0       HALI YA MAANDAMANO YA CHADEMA YALIYOPANGA KUFANYIKA JIJINI
MBEYA TAREHE 25.03.2013.

·         HALI NI SALAMA NA HAKUNA DALILI ZOZOTE ZA MAANDAMANO /VURUGU, WANANCHI WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZIKIWEMO ZA KIMAENDELEO KAMA KAWAIDA.

·         NAOMBA KUTUMIA FURSA HII KUWASHUKURU WANANCHI WOTE WA JIJINI MBEYA NA WILAYA ZOTE KWA KUWA WASIKIVUNA WATULIVU KWA KUWA AMANI,UTULIVUNA USALAMA NDIO NGUZO KUBWA KATIKA  KUPATA MAENDELEO.

·         NAWAPONGEZA VIONGOZI WA KITAIFA WA SERIKALI/JESHI LA POLISINA WA CHADEMA KWA MAKUBALIANO WALIYOFIKIA KWA MASLAHI YA TAIFA.
Signed By
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Post a Comment