Ads (728x90)

WANACHAMA WA SIMBA WAMNG’OA RAGE WAMTUHUMU KUTOWAJIBIKA

Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni kwenye mkutano huo.
Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi  wa sasa.
Mmoja wa wanachama akitoa maoni yake dhidi ya uongozi wa sasa.
Mwanachama mwingine akimchana ‘live’ Aden Rage kuhusu sakata la Mbuyu Twite na Kelvin Yondani.
Wanachama wakitoka kwa amani baada ya kumaliza mkutano.
Askari wakiangalia suala la usalama.  WANACHAMA wa klabu ya Simba, leo walifanya kikao cha dharura kwenye Hoteli ya Star Light Mnazi Mmoja jijini Dar na kuung’oa  uongozi wa klabu hiyo uliopo madarakani chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao.
 Wanachama hao wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha kiongozi aliyejiuzulu hivi karibuni, Zacharia Hans Poppe. Wanachama hao wamesema wanatarajia kuitisha mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu inayoendelea ili kuepusha kuivuruga timu.(CHANZO GLOBAL PUBLISHERS)

Post a Comment