Ads (728x90)

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI BW. SULEIMAN SULEIMAN AKIZUNGUMZIA UGUMU WA KUBADILISHA JINA LA SONGWE KUITWA JAKAYA KIKWETE

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE BW.SULEIMAN SULEIMAN AKIFAFANUA KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA UTARATIBU WA JINA LA VIWANJA VYA NDEGE VYA KIMATAIFA ULIVYO



WAZIRI WA UCHUKUZI DKT. MWAKYEMBE AKISAINI KITABU KATIKA ENEO LA UJENZI WA MAEGESHO KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MKOANI MBEYA

 
SIKU chache baada ya Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Mbeya (RCC) kupitisha jina la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe kuitwa jina la Jakaya Kikwete, Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini imetoa tamko juu ya mchakato wa ubadilishwaji wa jina unavyokuwa na kusema kuwa jina la uwanja wa ndege wa Kimataifa halibadilishwi kiholela.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege nchini Bw. Suleiman Suleiman aliyekuwepo katika ziara ya Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeulizwa kuhusu kubadilishwa kwa jina la  Songwe International Airport(SIA) na kuitwa jina la Jakaya Kikwete International Airport.

‘’Jina hili la SIA lipo katika ramani ya majina ya Viwanja vya ndege duniani, kubadilishwa jina ni hatua nyingine inayohitaji mchakato wa muda mrefu, kwa sasa tunadeal na ujenzi wa Uwanja wa ndege suala la jina si la msingi kwetu’’alisema.

Alisema kuwa vipo viwanja vingi vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini ambapo majina yao huratibiwa na kuingizwa katika mchakato wa siku 56 na kulipitisha kimataifa na kwamba jina hili la SIA lilifanyia taratibu zote na kutambulika kimataifa kwa namba HTGW.

Bw. Suleiman alisema kuwa kwa kutumia namba hiyo rubani yoyote duniani anajua anatua katika uwanja gani na kuwa ubadilishaji wa jina wa ghafla unaweza kugharimu utendaji wa Mamlaka kimataifa.

‘’Rubani yoyote duniani anajua jina la Songwe baada ya kujitambulisha kimataifa, kwa sasa tunaendelea kuboresha viwanja vyote vya ndege nchini ili viulingane na hadhi ya kimataifa,’’alisema Bw. Suleiman.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi Dkt. Mwakyembe aliwataka wananchi na wakazi wa mkoa wa Mbeya kutumia fursa ya kuwepo kwa uwanja huo kwa kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuzalisha mazao ya biashara na chakula katika ubora wa kimataifa.

Dkt. Mwakyembe ambaye pia alitumia fursa hiyo kutoa mifuko 100 ya saruji katika shule ya msingi ya Ikumbi iliyopo karibu na uwanja huo ambayo ilitolewa na kampuni ya db Shapriya inayojenga maegesho uwanjani hapo.


Post a Comment