Ads (728x90)

'' ONDOKENI HAPA HATUTAKI MTUPIGE PICHA MNAPOTOSHA UKWELI BADALA YA KUTETEA WANYONGE MNAPEWA VIJIELFU KUMI KUSALITI WANAFUNZI WANAONYIMWA HAKI ZAO,''NDIVYO ANAVYOSEMA MMOJA WA WANAFUNZI WA CHUO CHA AFYA CHA ST. AGREY KILICHOPO JIJINI MBEYA AMBACHO KINADAIWA KUTAPELI WANAFUNZI HAO WA MWAKA WA PILI AMBAO WANATAKIWA KUFANYA MTIHANI MWEZI WA NANE, HADI SASA HAIJULIKANI HATIMA YAO KUTOKANA NA CHUO HICHO KUKOSA VIGEZO VYA KITAALUMA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOTIMIZA MASHARTI YA USAJILI WAO.

BANGO LA CHUO HICHO KAMA LINAVYOJIELEZA

KAIMU OFISA UPELELEZI MKOA WA MBEYA AKISIKILIZA KERO ZA WANACHUO HAO AMBAO WALIPANGA KUANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA WA MBEYA KUPELEKA KILIO CHAO CHA KUTAPELIWA NA CHUO HICHO

ASKARI POLISI WAKIJADILIANA JAMBO BAADA YA KUSIKIA KERO ZA WANACHUO HAO


MAJENGO YA CHUO HICHO AMBACHO KINADAIWA KUTOFUATA MASHARTI YA USAJILI NA KUSABABISHA WANACHUO KUTOFANYA MTIHANI WAO WA MWEZI WA NANE PAMOJA NA KULIPIA ADA YA ZAIDI YA SH. MILIONI 2 KWA KILA MWANAFUNZO WA CHUO HICHO


WANAFUNZI WA CHUO CHA AFYA ST.AGREY WAKIWA WAMEKUSANYIKA MBELE YA CHUO HICHO WAKITAFAKARI HATIMA YAO BAADA YA KUDAI WAMETAPELIWA NA CHUO

GARI YA MENEJA WA CHUO HICHO AMBAYE ALIFIKA HAPO CHUONI KINYEMELA NA KUONDOKA KWA NJIA ZA PANYA BAADA YA KUKUTANA NA KUNDI LA WANACHUO WAKISHINIKIZA KUREJESHEWA FEDHA ZAO AU KUTAFUTIWA CHUO KINGINE CHA KUFANYIA MTIHANI BAADA YA CHUO HICHO KUKOSA SIFA

MWANAMAMA HUYU MAKAMU MKUU WA CHUO AKITAFAKARI JAMBO BAADA YA KUSIKIA MALALAMIKO YA WANAFUNZI WA CHUO HICHO

''WAZAZI WETU WAMEUZA NG'OMBE ILI SISI TUSOME, TUMELIPA MILIONI 2.5 LEO TUNAAMBIWA HATUWEZI KUFANYA MTIHANI BAADA YA CHUO HIKI KUTOKUWA NA VIGEZO, TUTAENDA WAPI SISI, TUNAOMBA SHERIA IFUATE MKONDO WAKE,''NDIVYO AMBAVYO ANAONEKANA KUSEMA MMOJA WA WANAFUNZI WA CHUO HICHO KWA MSISITIZO.
 

''HAWA WATU HAWANA HURUMA HATA CHEMBE, HIVI WANGEKUWA WATOTO WAO WANGEWEZA KUWAFANYIA HIVI? ALISEMA KIJANA HUYU
 
''NGOJA NISEPE TARATIIBU HAWA WANAFUNZI NI NOOMA!!!''...MENEJA WA CHUO HICHO AKITAFUTA UPENYO WA KUTIMUA CHUO HAPO BAADA YA SEKESEKE LA WANAFUNZI KUPAMBA MOTO''
''HAPA UPEPO UMEKAA VIZURI NAWEZA KUWAZUGA NA KUSEPA KIMTINDO'' NDIVYO ANAVYOONEKANA MENEJA WA CHUO HICHO
 

BAADA YA SAKATA HILO CHUONI HAPO HATIMAYE MENEJA WA CHUO ALITOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA, NDIPOMMSALA ULIPOWAANGUKIA WANAHABARI WALIOFIKA CHUONI HAPO NA KUDAIWA KUWA WAO WANATUMIWA NA WANACHUO HAO KUTOA TAARIFA ZA UONGO NA KUWAZOMEA NA KUWAKATALIA KUWAPIGA PICHA PAMOJA NA JITIHADA ZA WANAHABARI HAO KUJITETEA JUU YA HILO
 
WANACHUO HAO WALIENDA MBALI ZAIDI NA KUTOA MOJA YA MAGAZETI YANAYOTOLEWA KWA WIKI AMBALO LILIKUWA LIKIELEZEA UBORA WA CHUO HICHO, JAMBO AMBALO WANACHUO HAO WALIPINGA NA KUWATUPIA LAWAMA WANAHBARI KWAMBA WAMENUNULIWA KWA AJILI YA KUUFICHA UKWELI.


NA SISI NDIO TUNALIPA FEDHA CHUONI HAPO, KWANINI MNAKUBALI KUNUNULIWA WA VIJIELFU KUMI KUMI, WANGEKUWA WATOTO WENU MNGEKUBALI KUANDIKA UJINGA HUU?" NDIVYO AMBAVYO WALIONEKANA KUSEMA NA HATA KUSABABISHA MWANDISHI WA BLOGU HII KUPANDA JAZBA KUTOKANA NA WANAFUNZI HAO KUKOSA DISPLIN! KWA KUTOA MANENO YA KEJELI KWA WANAHABARI.
SIKILIZENI NYINYI SIE KILA MWANAHABARI ANATUMIWA WENGINE TUPO KWA AJILI YA KUWASAIDIA MATATIZO YENU HEBU KUWENI WASTAARABU, SISI NDIO KISEMEO CHENU KILIO CHENU NANI ATAKISIKILIZA BILA SISI" ALIONGEA MWANDISHI WA BLOGU HII AMBAPO HATA HIVYO ALIENDELEA KUZOMEWA NA KUELEZWA KUWA HANA TOFAUTI NA YULE ALIYEANDIKA TAARIFA ZILE KWA KUWA TANGU KILIO HICHO KIMEANZA KUTOLEWA NA WANACHUO HAO WANAHABARI WANAFIKA CHUONI HAPO WANAINGIA KWA MENEJA WA CHUO KISHA WANAONDOKA KIMYA KIMYA BAADA YA KUKATIWA MSHIKO.
WANAFUNZI HAO BAADA YA KUONA KUWA HAKUNA MSAADA WOWOTE WANAOUPATA WALIAMUA KUANDAMANA HADI KWENYE OFISI YA MKUU WA WILAYA YA MBEYA KWA AJILI YA KUTOA KILIO CHAO NA BAADAYE KUKUTANA NA OFISA TAWALA WA WILAYA GEOFREY ANANIA AMBAYE ALIWAAMBIA KUWA SUALA LAO LINASHUGHULIKIWA ILI KUPATIWA UFUMBUZI.

Post a Comment