Ads (728x90)

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKITAFAKARI JAMBO PAMOJA NA BAADHI YA ASKARTI POLISI MJINI TUNDUMA KUFUATIA VURUGU ILIYOIBULIWA LEO ASUBUHI JUU YA SAKATA LA UCHINJAJI KATI YA WAKRISTO NA WAISLAMU

WANAHABARI WAKIWA WAMEJIBANZA KATIKA KITUO CHA POLISI MJINI TUNDUMA


ASKARI WA KIKOSI CHA MBWA WAKIJIANDAA KUKABILIANA NA LOLOTE KATIKA VURUGU HIZO





ASKARI POLISI MARA BAADA YA KUWATAWANYA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO WALIOSHINIKIZA KUFUNGWA KWA MABUCHA YA WAISLAMU








KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa ni waumini wa dini ya Kikristo jana wamedaiwa kuvamia bucha za nyama zinazomilikiwa na waislamu na kulazimishwa kufungwa kwa bucha hizo kutokana na madai ya kuwekwa kwa uwiano sawa wa uchinjaji baina ya waislamu na wakristo.
Kundi hilo la waumini walikuwa wakipita katika barabara kadhaa za mji mdogo wa Tunduma kushinikiza kufunguliwa kwa mabucha ya wakristo na  kuibua taharuki kwa baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo hayo ambao walilazimika kufunga maduka baada ya askari kuanza kurusha mabomu kutawanya watu hao.
Vurugu hizo ambazo ziliambatana na vijana hao kuziba barabara na kuchoma matairi zilianza kutawanya kwa mabomu ya machozi ilhali kundi hilo la watu nalo lilianza kuwarushia mawe askari waliokuwemo kwenye magari ya doria na kusababisha askari mmoja aliyekuwa akiendesha gari la polisi kujeruhiwa.
Kutokana na hali hiyo mpaka wa Tanzania na Zambia ulilazimika kufungwa ili kupisha vurugu hizo ambazo zimedumu kuanzia saa 4;00 asubuhi mpaka majira ya saa 11 jioni.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ambaye alifika kwenye eneo la tukio alisema kuwa vurugu hizo zinaonekana kuwa na ushawishi wa kisiasa kutokana na ukweli kuwa hazikupaswa kufikia hatua hiyo.
Kamanda Athumani amesema kuwa jeshi la polisi linawatafuta Mchungaji wa kanisa la KKKT la mjini Tunduma aliyefahamika kwa jina la Gidioni Mwamafupa na Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka kutokana na kudaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine juu ya kutokea kwa tukio hilo.
Amesema kuwa mbali na watu hao jeshi la polisi linawashikilia zaidi ya watu 40 ambao wanaendelea kusakwa kutokana na kusababisha vurugu hizo ambazo zimesababisha kukwamishwa kwa shughuli mbalimbali za kibiashara mjini humo.
Awali inadaiwa kuwa baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo walipeleka barua kwenye uongozi wa serikali ya mji huo wakitaka wapewe ridhaa ya kuchinja kama vile ambavyo waumini wa dini ya kiislamu wanafanya.
Katika madai yao ambayo yalimfikia mkuu wa wilaya hiyo Abihudi Saideya walihitaji kupata kibali cha kuchinja ambapo hata hivyo kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya yalilikuwa yakifanyiwa kazi ngazi ya Taifa.
Amesema kuwa hata hivyo waumini hao walianza kuchinja kabla hawajapewa kibali cha serikali na kusababisha kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi baina ya waumini wa dini hizo.

Post a Comment