Ads (728x90)

KATIBU WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA SADY MWANG'ONDA AKIZUNGUMZIA MIKAKATI YA WASANII KUJIKWAMUA KATIKA KAZI ZAO ZA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA

BAADHI YA WASANII WA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO ULIOWAKUTANISHA WAIGIZAJI KATIKA UWANJA WA CITY PUB JIJINI MBEYA


MWENYEKITI WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI MKOA WA MBEYA SAMWEL MWAMBOMA AKIZUNGUMZA AZMA YA KUWAKUTANISHA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYABAADHI YA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA WAKIWA WAMESIMAMA DAKIKA MOJA KWA AJILI YA KUMKUMBUKA MSANII MWENZAO STEVEN KANUMBA ANAYETIMIZA MWAKA MMOJA TANGU AFARIKI DUNIA APRIL 7 MWAKA JANA


WASANII WA SANAA YA UIGIZAJI MKOANI MBEYA WAMEKUTANA NA KUUNDA SHIRIKISHO LA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA KWA NIA YA KUBORESHA KAZI ZAO ZA SANAA AMBAZO KWA MIAKA MINGI ZIMEKUWA HAZIWANUFAISHI WAIGIZAJI WENYEWE.
WAIGIZAJI HAO WAPATAO 234 WALIKUTANA LEO MCHANA KATIKA UWANJA WA CITY PUB ULIOPO MAFIAT JIJINI MBEYA NA KUELEZEA CHANGAMOTO MBALIMBALI WANAZOKUTANA IKIWA NI PAMOJA NA KAZI ZAO KUTOTHAMINIWA NDANI NA NJE YA NCHI.AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO KATIBU WAQ MUDA WA SHIRIKISHO HILO SADY MWANG'ONDA ALISEMA KUWA VIPAJI VYA KAZI ZA SANAA VINAKUFA MIONGONI MWA WAIGIZAJI HAO KUTOKANA NA KAZI HIZO KUTOJULIKANA.
ALISEMA KUWA WAIGIZAJI WENGI WA MKOA WA MBEYA WANARIDHIKA KUONA KAZI ZAO MAJUMBANI MWAO BADALA YA KUZITANGAZA KWA JAMII ILI ZITOE MAFUNDISHO KWA JAMII NA KUJIONGEZEA KIPATO.ALISEMA KUWA KAZI YA UIGIZAJI NI SAWA NA KAZI NYINGINE HIVYO INATAKIWA KUFANYWA KWA WELEDI NA UMAKINI KWA KUZINGATIA KIPAJI NA ELIMU.
MWANG'ONDA ALISEMA KUWA WAIGIZAJI WENGI HAWANUFAIKI NA KAZI ZAO HUKU WENGINE WAKIJIKUTA WAKIIGA KAZI ZILIZOIGIZWA MIAKA MINGI KUTOKANA NA WAIGIZAJI HAO KUTOKUWA WABUNIFU.
ALISEMA KUWA ILI KUBORESHA KAZI ZA UIGIZAJI KUNAHITAJI USHIRIKIANO BAINA YA WAIGIZAJI,MADIRECTOR NA MAPRODYUZA NA KWAMBA NI VYEMA KWA SASA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA WAKATUMIA FURSA YA MKOA WAO KUFANYA KAZI ZINAZOKUBALIKA KATIKA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA.
ALIFAFANUA KUWA MKOA WA MBEYA UNA FURSA NYINGI ZA VIPAJI KWA WASANII AMBAO WAKITUMIA VYEMA VIPAJI NA FURSA ZILIZOPO, MKOA WA MBEYA UNAWEZA KUWA NI SEHEMU YA KIVUTIO KWA KAZI ZA UIGIZAJI ZITAKAZOTOKEA MKOANI HUMO.
STORI NA RASHID MKWINDA
Post a Comment