Ads (728x90)

BAADHI YA NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA MKOANI ARUSHA ZILIZOJENGWA NA KUUZWA KWA WANANCHI

NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA ZILIZOPO KATIKA ENEO LA MERU JIJINI ARUSHA

MAJENGO YA SHIRIKA LA NYUMA LA TAIFA YALIYOPO KATIKA ENEO LA LEVELOSI, NYUMBA HIZI ZIMEJENGWA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NA KUUZWA KWA WANANCHI NA BAADHI YAKE KUPANGISHWA


OFISI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA ILIYOPO KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA

NYUMBA 100 zimejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)mkoani Arusha ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la wakazi na kukua  kwa kasi kwa Jiji hilo la kitalii lililopo mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya.
Idadi hiyo ya nyumba ni kati ya nyumba za makazi 98 zilizopo katika eneo la Levolosi na Meru ikiwa ni mpango wa Taifa wa shirika hilo kujenga jumla ya nyumba 15,000 kwa kuanzia mwaka 2010 - 2015.
Akizungumza juu ya mkakati wa shirika hilo kuborsha makazi ya wakazi wa jiji hilo Meneja wa mkoa wa NHC mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika alisema kuwa asilimia 30 ya nyumba hizo zitapangishwa na nyingine zitauzwa kwa wananchi kulingana na mahitaji na hali zao za kiuchumi.
‘’Nyumba zetu zimejengwa na kuuzwa kwa madaraja ya watu wa zote,watu wa hali ya kawaida, wa kati na wa hali ya juu,’’alisema Bw. Kisarika.
 Alisema kuwa hadi sasa Shirika limebakisha jumla ya nyumba 38 ambazo baadhi yake zitapangishwa na nyingine zitaendelea kuuzwa kulingana na mahitaji ya wanunuzi.
Bw. Kisarika alisema kuwa shirika litaendelea kuboresha nyumba zake kwa kuzibomoa na kujenga upya ambapo wapangaji waliopo katika nyumba hizo watahamishiwa katika nyumba mpya za shirika.
Kwa upande wake Ofisa mauzo na masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoani humo Bw.Gibson Mwaigomole alisema kuwa shirika limeamua kuboresha makazi ya Jiji la Arusha kwa kuongeza majiji mengine mawili ambayo yatakuwa na nyumba bora za kisasa.
Alisema kuwa shirika limetenga jumla ya hekari 900 katika maeneo mawili ya USA River lililopo km 18 kutoka katikati ya Jiji lenye hekari 600 na Safari lililopo eneo la Matevesi km 10  kutoka katikati ya jiji lenye jumla ya hekari 300 na kwamba mara mradi utakapoanza nyumba mpya za kisasa zitaanza kujengwa.

Post a Comment