Ads (728x90)


MGOMBEA WA NAFASI MBILI ZA UENYEKITI NA MAKAMU WA MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA JACKSON NUMBI AKIREJESHA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI KWA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI BRANDY NELSON ANAYESHUHUDIA NI MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI MOSES NG'WAT

MGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA JACKSON NUMBI AKITIA SAINI BAADA YA KUREJESHA FOMU KATIKA OFISI ZA KLABU LEO MCHANA

MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI MOSES NG'WAT AKIMPONGEZA MGOMBEA UENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA JACKSON NUMBI MARA BAADA YA KUREJESHA FOMU LEO MCHANA


MGOMBEA NAFASI YA UJUMBE WA KLABU YA MBEYA PRESS FURAHA ELIABU AKIREJESHA FOMU ZA NAFASI HIYO KWA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI BRANDY NELSON LEO MCHANA, (PICHA CHINI), MGOMBEA NAFASI YA UJUMBE WA KLABU FURAHA ELIABU AKITIA SAINI MARA BAADA YA KUREJESHA FOMU YA KUWANIA NAFASI HIYO LEO MCHANA
BAADHI YA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WAMEANZA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI KUFUATIA KUONDOLEWA KWA UONGOZI WA AWALI AMBAO ULIKUMBWA NA MADAI YA  HUJUMA ZA KUGHUSHI NYARAKA NA KUTAFUNA MAMILIONI YA FEDHA ZA KLABU HIYO.

KWA MUJIBU WA MWENYEKITI TUME YA UCHAGUZI YA KLABU HIYO BRANDY NELSON WALIOJITOKEZA HADI SASA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NI WANACHAMA WANNE AMBAPO HADI SASA WALIOREJESHA NI WATU WATATU.

ALIWATAJA WALIOJITOKEZA KUCHUKUA FOMU NA KUREJESHA NI PAMOJA NA JACKSON NG'UMBI ANAYEWANIA NAFASI MBILI ZA UENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI NA FURAHA ELIABU AMBAYE ANAWANIA NAFASI YA UJUMBE.

KWA MUJIBU WA MWENYEKITI HUYO WA TUME NI KWAMBA MWISHO WA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU NI MEI 18 AMBAPO UCHAGUZI UNATARAJIA KUFANYIKA MEI 25 MWAKA HUU.

ALISEMA KUWA WATAKAOHUDHURIA KATIKA UCHAGUZI HUO NI WANACHAMA HAI PEKEE AMBAO WAMELIPA ADA YA MWAKA NA KWA WALE WALIOCHELEWA KULIPA ADA HAWATARUHUSIWA HADI HAPO UCHAGUZI UTAKAPOISHA NA VIONGOZI WAPYA WATAKAPOPATIKANA.

Post a Comment