Ads (728x90)

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKIINGALIA MIILI YA WASHUKIWA WA UJAMBAZI KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

MIILI YA WASHUKIWA WA UJAMBAZI KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKIONESHA GARI LILILOKUWA LIKITUMIWA NA WASHUKIWA WA UJAMBAZI WALIOUAWA KATIKA MAPIGANO NA JESHI LA POLISI

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUIMANI AKIWA NA SILAHA ZINAZODAIWA KUTUMIWA NA WASHUKIWA WA UJAMBAZI

KIKOSI KAZI KILICHOFANIKISHA KUUAWA KWA WASHUKIWA WA UJAMBAZI KATIKA ENEO LA GARIJEMBE MKOANI MBEYA
WATU watano wenye silaha wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao hawajatambulika majina yao wameuawa jana mchana katika kijiji CHA Galijembe nje kidogo ya Jiji la Mbeya baada mapambano ya kurushiana risasi kati yao na askari polisi wa mkoa huo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana jioni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani amesema kuwa watu hao ambao walikutwa na bunduki mbili aina ya SMG yenye risasi 16 na  MARK III yenye risasi mbili katika magazine.
Kamanda Diwani amesema kuwa watu hao waliokuwa katika gari yenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio walikuwa na dalili za kufanya mauaji na uhalifu mkubwa katika maeneo ya Tukuyu,Ushirika na Uyole.
Amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia Jeshi la Polisi lilifuatilia neyndo za watu hao katika maeneo mbalimbali ili kuzuia tukio lolote la mauaji na uhalifu ambao ungeweza kutokea katika siku mbili hizi.
Kamanda Diwani amesema kuwa wakiwa katika doria ya kawaida walilisimamisha gari lililokuwa na washukiwa hao wa ujambazi ambapo lilisimama vizuri na baadaye ghafla watu wawili walitoka nje ya gari na kurusha ovyo risasi wakielekeza eneo ambalo walikuwepo askari polisi.
Amesema hata hivyo risasi zao hazikuweza kuwakuta askari polisi bali watu hao watano walijeruhiwa kwa risasi katika maeneo mbalimbali ya miili yao na baadaye kufariki dunia wakiwa katika hospitali ya rufaa ya Jijini Mbeya.
Amesema kuwa mbali na bunduki mbili walizokutwa nazo walikuwa na kamba maalumu ambayo inatumiwa kwa namna mbalimbali za uhalifu ikiwemo kuwafunga watu waliotekwa na baadhi ya mizigo watakayoiba na kwamba kamba hiyo haikatiki kwa urahisi.


Post a Comment