Ads (728x90)


SIKU CHACHE BAADA YA MALALAMIKO YA MWANAMUZIKI LADY JAY DE DHIDI YA KITUO CHA RADIO CHA CLAOUDS FM NA MKURUGENZI WAKE RUGEMALILA MUTAHABA HATA KUTANGAZA HADHARANI KWA KUTOA WOSIA MZITO WA KUMPIGA MARUFUKU RUGE KUTOHUDHURIA MAZISHI YAKE IWAPO ATAFARIKI DUNIA.

LADY JAY DEE AU MAARUFU KWA JINA LA BINT MACHOZI AU KOMANDOO KAMA ANAVYOFAHAMIKA MIONGONI MWA WAPENZI WAKE ALIFIKIA HATUA HIYO BAADA YA MADAI YA KUWEKEA KAUZIBE JUU YA MAENDELEO YAKE YA KIMUZIKI NA KUTAKA KUUPOTEZA UMAARUFU WAKE.

KATIKA MAZUNGUMZO YAKE KUPITIA MTANDAO JIDE ALIKARIRIWA AKISEMA KUWA LENGO LA CLOUDS FM KUMUONA AMEANGUKA NA ANAPOTEA KATIKA RAMANI YA MUZIKI NA KWAMBA UAMUZI WAKE NI KUKATAA KUBURUZWA NA KUDAI KUWA KINACHOFANYIKA KWA CLOUDS NI KUWA HAKUNA MSANII AMBAYE ANAWEZAKUFANYA VIZURI BILA CLOUDS FM.

ALISEMA KUWA UMAARUFU WAKE HAUKUTOKANA NA CLOUDS FM BALI JITIHADA ZAIKE BINAFSI NA KWAMBA IWAPO WAO WALIMBEBA BASI WALIPASWA KUWABEBA DADA ZAO WALIOZALIWA NAO TUMBO MOJA ILI WAWEZE KUIMBA NA KUFIKIA UMAARUFU WANAODAI UMETOKANA NA  CLOUDS.
‘’KAMA KWELI WEWE KUSAGA UNAJUA KUBEBA BASI BEBA JIWE LIIMBE LIWE STAR’’ALISEMA JIDE.

KATIKA KUONESHA KUWA AMEKERWA ZAIDI JIDE ALINUKULIWA AKISEMA KUWA HATA SIKU AKIFA CLOUD FM WASIPIGE NYIMBO ZAKE NA WALA KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA KUWA IWAPO WATAJITOKEZA WATU HAO KATIKA MAZISHI YAKE WAPIGWE MAWE.
MARA BAADA YA KAULI HIYO RUGE KUPITIA KIPINDI CHA POWER BREAKFAST KINACHORUSHWA NA CLOUDS FM ALIAMUA KUKATA UKIMYA NA KUELEZEA HALAI HALISI JUU YA MGONGANO HUO.

 RUGE ALISEMA KUWA CLOUDS WALIMPA SAPOTI KUBWA SANA KIMUZIKI IKIWEMO NA KUSAIDIA ALBUM YAKE YA KWANZA YA MACHOZI NA KWAMBA YEYE NDIYE ALIYEMSHAURI LADY JAY DEE PAMOJA NA BAADHI YA WANAMUZIKI WENZIE KAMA VILE RAY C NA SOGGY DOGGY KUACHANA NA UTANGAZAJI NA KUJIKITA ZAIDI KWENYE MUZIKI.
KUHUSU MALALAMIKO YA KUITANGAZA ZAIDI BENDI YA SKYLIGHT RUGE ALISEMA KUWA BENDI HIYO SI MALI YA JOSEPH KUSAGA MKURUGENZI WA CLOUDS FM WALA YEYE BALI BENDI HIYO NI MALI YA SEBASTIAN NDEGE NA KUONGEZA KUWA IWAPO UPO MVUTANO WA BAINA YA MACHOZI BAND NA SKYLGHT UTAKUWA NI MVUTANO WA KIBIASHARA KWANI BENDI ZOTE ZINALIPIA MATANGAZO KWENYE RADIO HIYO.
RUGE ALISISITIZA KUWA RADIO HIYO NI BINAFSI HIVYO INA UAMUZI WAKE BINAFSI WA KUPIGA NA KUACHA BAADHI YA NYIMBO NA KWAMBA WANAOWAKEJELI WANAPASWA KUKUMBUKA WALIKOTOKEA KABLA HAWAJAPATA UMAARUFU WALIONAO.

Post a Comment