MSEMO WA
KUFA KUFAANA ULIDHIHIRIKA JANA MAJIRA YA SAA MOJA NA NUSU KATIKA KIJIJI CHA
KING’ORI KILOMITA 5 KUTOKA JIJINI ARUSHA BAADA YA LORI LENYE NAMBA ZA USAJILI T 284 AZG KUANGUKA NA
KUMWAGA MAFUTA YALIYOMO KATIKA MATENKI YA GARI HILO NA KUSABABISHA WANANCHI WA
KIJIJI HICHO KUGOMBEA MAFUTA HAYO KILA MMOJA AKIWA NA CHOMBO CHAKE.
BILA KUJALI
HATARI AMBAYO INGEWEZA KUTOKEA KILA MKAZI WA KIJIJI KILE WAKIWEMO AKINA
MAMA,WATOTO VIJANA NA WAZEE WALIMIMINIKA ENEO HILO NA KUCHOTA MAFUTA HAYO MITHILI
YA WATU WALIOKUWA WAKICHOTA MAJI KISIMANI.
WANANCHI HAO
WALIONEKANA WAKIWA WAMEBEBA MAGUDURIA MAKUBWA NA MADOGO KILA MMOJA KULINGANA NA
UWEZO WAKE NA KUKINGA MAFUTA HAYO KATIKA AMOJA YA TENKI LILILOKUWA LIKIBUBUJIKA
MAFUTA KWA WINGI HUKU BAADHI YAO WAKIONEKANA WAKICHOTA YALIYOMWAGIKA CHINI KWA
MIKONO NA BAADHI YAO KWA VIKOMBE.
AIDHA TUKIO
HILO LILISABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI YALIYOKUWA YAKIELEKEA ARUSHA NA
YALE YALIYOKUWA YAKITOKA ARUSHA KUELEKEA MIKOA MINGINE BAADA YA BASI AINA LA
DAR EXPRESS LENYE NAMBA ZA USAJILI T 152 BDQ KUTAKA KUPITA ENEO HILO NA BAADAYE
KUSHINDWA BAADA YA KUTELEZA KWENYE MAFUTA NA KUZUIA KABISA NJIA.
KADRI MUDA ULIVYOZIDI KUENDELEA NDIVYO AMBAVYO
UMATI WA WATU WALIENDELEA KUMIMINIKA ENEO HILO AMBAPO HATA BAADHI YA WENYE
MAGARI WALILAZIMIKA KUSHUKA NA MAGUDURIA KUKINGA MAFUTA HAYO KWA AJILI YA
MATUMIZI YA MAGARI YAO. |
Post a Comment