Ads (728x90)


Mungai kwa tume ya Elimu
BARUA YA WAZI YA Joseph J.Mungai( MB mstaafu ) P.O.BOX 34 Mafinga S: 0753 192999 BP: jjmungai@tatepa.com BARUA YA WAZI KWA TUME YA ELIMU YA KUFELI 60% MTIHANI WA KVI 12012 ILIYOTEULIWA NA MHE WAZIRI MKUU 29/03/2013 Kumb Na. JJM/2013/ELIMU/19 Kwa Mwenyekiti Tume ya Elimu ya Kufeli KIV Ofisi ya Waziri Mkuu DAR ES SALAAM Ndugu Mwenyekiti KUONGEZEKA WANAOFELI KIV KUTOKA 9.7% MWKA 2007 HADI 60% 2012 1.1 Nnawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau fwa elimu kuwaletea maoni na au/ushauri. 2.0 Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi na kuziendesha kwa mika zaidi ya 10 Sekondari 9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani ( 3) Itengule ( 4) Igowole ( 5) Itandula ( 6) Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni mwaka 2000 hadi 2005. 3.0 Kabla ya kutoa ushauri naoba kuipa Tume yako ufahamu wa ukweli ufuatao: 3.1 Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0) mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%!!!!! 3.2 Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%, 2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi 2007 ni 10%. Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka 2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in Education, National Data) ya miaka husika. 3.3 Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne walikuwa wastani wa 10% ambayo inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka kila mwaka hadi kufikia 60% ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada ya matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya “utafiti kudadisi sababu za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”, lakini hadi leo haikusomwa. Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja isiyo ya siri ya ndani ya wizara ya Elimu. 4.0 Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo yanaweza kusomwa katika maandiko mawili ya Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa maboresho hayo uzito w akisheria yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla ya wakati wake. Maboresho yamewekwa kando moja baada ya jingine au hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi ilivyokuwa kabla ya mwaka 2000. USHAURI: 5.0 Kwa kuwa Elimu ni nyenzo muhimu sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kucho cchea maendeleo ya nchi nimeamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo: 5.1 Utaratibu sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression) uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe bila kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza, la pili na la Tatu ambayo Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka ya kukalilisha, kama mwanafunzi hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu. 5.2 Tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu niliyoyataja akatika 4(a) na (b) hapo juu yaliyomo maboresho ya elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha kufaulu vizuri katika Elimu ya Msingi na Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya kutumia muda mwingi na fedha n=yingi kugundua upya gurudumu. 5.3 Taasisi ya Elimu Tanzania ( Tanzania Institute of Education –TIE) iagizwe na iachiwe kutekeleza wajibu wake wa kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala. 5.4 Wanasiasa tuache kuamua bila kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri w kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu. Kutokana na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama hayo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “ anayeficha maradhi kifo kitamuumbua” Wasalamu BARUA Joseph J Mungai MB mstf MDAU WA ELIMU) KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN


Post a Comment

  1. Yote aliyosema Mungai siyakatai lakini haya ni mavuno ya aliyoyapanda yeye na wenzake walipopewa majukumu.Nasema hayo kwa sababu zifuatazo;
    1-Ni kigezo gania alichokitumia cha kuviua vyou vya ualimu vya Mkwawa na Ifunda kuwa tawi la cguo kikuu na Sekondari ya wasichana wakati ameanzisha shule za kata zenye uhitaji wa walimu.
    2-Alitumia kigezo gani kuvuruga mitaala iliyokuwepo ya michepuo na kuwahamisha walimu pamoja na watumishi kwenda wasikokuwa na uwezo nako.Mfano walimu wa ufundi Tanga tech kuhamishiwa mashule ya kawaida wakati hata hayo masomo wanakokwenda kufundisha hawakuyasomea
    3-Alitumia kigezo gani kuua shule za vipaji maalumu za Illibolu,Mzumbe,Iyunga,Ifunda,Kibaha,nk kwa kuondoa baadhi ya mikondo ya kidato cha nne na kuingiza mikondo ya kidato cha tano wakati mahitaji ni mengi kwa hili kundi la kwanza la kidato cha nne.
    4-Ni kwa nini alikuwa anawacheleweshea stahiki zao walimu na watumishi wa sekondari
    5-Ni wapi iliipeleka ile mitaala ya kwanza aliyoikuta wakati wa waliomtangulia pale wizarani na kuchapisha ya kwake na kuleta vitabu vyake vya kiada .
    6-Hivi alitegemea nini kitatokea kama yeye na wenzie waliigeuza waizara ya Elimu kama mali yao na kuwahamisha ovyo walimu na wengine kuwatimua pale anapouliza ama kutetea maslahi ya walimu.
    INA MAANA ALIKUWA HUJI ANAPANDA MBEGU YA KUFELI KWA WANAFUNZI ASITUDANGANYE

    ReplyDelete