Ads (728x90)TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14. 08. 2013.


WILAYA YA MBOZI – MAUAJI

MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00 HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO.  MAREHEMU ALIVIZIWA WAKATI   AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA NDOANO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  MAZUNGUMZO  NA  YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI

MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:05 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI, MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KANGA.  CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA MATATIZO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.Imesainiwa na,
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Post a Comment