Ads (728x90)

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akijiandaa kuuzindua wa maonesho ya Kilimo Nane Nane jijini Mbeya


Katibu wa TASO kanda Ramadhani Kiboko akisoma taarifa kabla ya uzinduzi wa maonesho ya Kilimo Nane Nane Jijini Mbeya

Baadhi ya Makatibu tawala kutoka mikoa sita inayojumlisha nyanda za Juu kusini wakiwa katika uzinduzi wa maonesho ya Nane Nane Jijini Mbeya





Katibu wa TASO Kanda Ramadhani Kiboko akikabidhi taarifa ya TASO kwa mgeni rasmi, Dkt. Harrison Mwakyembe



Kikundi cha Sarakasi kikionesha burudani katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nane Nane





Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Asery Msangi akizungumza wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane Nane



Dkt. Mwakyembe akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa sherehe maonesho ya Kilimo Nane Nane


.

WAZIRI wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa siku tisini kuondolewa matrekta yanayofanyakazi bandarini na badala yake yapelekwe vijijini ili yasaidie kufanya shughuli za kilimo.
Dkt. Mwakyembe aliyasema hayo leo mchana wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Kilimo Nane Nane ambayo yanajumuisha mikoa sita ya nyanda za juu kusini na kufanyika Jijini Mbeya.
Alisema kuwa wakulima wamekuwa wakipata shida nyenzo za kilimo ilhali bandarini kuna matrekta yanayopakua mizigo kinyume na kazi zake za kilimo.''
Kwa kuwa hili jambo lipo mikononi mwangu nitalishughulikia ipasavyo, naagiza miezi mitatu hadi Oktoba yawe yameondoka pale bandarini''alisema Dkt. Mwakyembe.Alisema kuwa atatoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vye usalama kuhakikisha matrekta yote yanaenda vijijini badala ya kuzagaa mijini kwa kazi ambazo hazina manufaa kwa Mkulima.
''Nataka Matrekta yalime sio kubeba mizigo bandarini,''alisisitiza.
Aidha Dkt. Mwakyembe  aliwataka wakulima kuboresha mbinu za uzalishaji kwa kulima kilimo cha kisasa kwa kuwatumia wataalamu ili kuongeza tija na kipato.
Alisema kuwa azma ya uzalishaji inahitaji mazingira yaliyowezesha na kwamba serikali imeongeza kasi kuboresha miundo mbinu katika mwaka wa fedha wa 2013 ambapo jumla ya sh. Bilioni 162.5 zimetengwa kwa miradi ya umeme kuanzia mwezi Oktoba zitakazochochea uanzishwaji wa miradi.

Pia Dkt. Mwakyembe alisema kuwa serikali imetenga jumla ya sh.Bilioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa barabara za vijijini ili kuboresha shughuli za kilimo ambapo barabara kuu za kiwango cha lami zinazounganisha mikoa ya Ruvuma, Katavi na Rukwa zinaendelea kutengenezwa.




Post a Comment