Ads (728x90)

MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa wilaya ya Kyela imewaachia kwa dhamana washitakiwa sita wa makosa manne ya ikiwemo kula njama, kufanya vurugu, kutenda kosa na kujeruhi.
 Washitakiwa hao Ibrahimu Shaaban(17),Ambokile Mwangosi919), Sadick Abdul(28),Mashaka Kassim(30),Ahmad Kassim(30) na Issa Juma(37)walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa dhamana yao iliyokataliwa na mwendesha mashtaka Nicolaus Tiba mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Joseph Luambano.
Awali washitakiwa hao walaidaiwa kumpiga Shekhe Nuhu Mwafilango wakati akiwa katika sijida wakati akiswalisha ibada ya swala ya Id el fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa wa wilaya ya Kyela.


Post a Comment