Ads (728x90)


Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo Gospel Kitaa imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

Gospel Kitaa itaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.Kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola ingia hapa....(stori kwa hisani ya Gospel Kitaa)

Post a Comment