Ads (728x90)



MILIONI 22 ZACHANGANYWA KUIPIGA TAFU KIMONDO
WADAU wa soka wilayani Mbozi na Momba juzi jioni walifanya harambee na kiukusanya jumla ya sh. milini 22 kwa ajili ya kuipiga tafu timu ya Kimondo ambayo imepanda ligi kuu ya daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 14.
Harambee hiyo ambayo pia iliwahusisha viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA)ilifanyika katika ukumbi wa Shimoni uliopo mjini Vwawa ambapo mbali na michango hiyo wadau walitaka kuunganisha nguvu ili timu hiyo iweze kufanikiwa kufuzu kucheza ligi kuu mwakani.
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala alisema kuwa uongozi wa mkoa wa Mbeya utaendelea kufanya jitihada kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri ili kuweka historia ya mkoa wa Mbeya kupandisha timu kila mwaka.
Alisema kuwa mkoa wa Mbeya una wachezaji wengi wenye vipaji ambavyo vikitumiwa vyema mkoa utarejea katika ramani ya soka kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Katibu wa chama mpira wa miguu wilaya ya Mbozi, (MBOFA)William Mwamlima alisema kuwa timu ya Kimondo imekumbana na changamoto nyingi hadi ilipofikia hatua hiyo hivyo jitihada za ziada zinahitajia kuisaidia timu hiyo ili iweze kushinda na kucheza ligi kuu.
Alisema kuwa jumla ya sh. milioni 92 zinahitajika kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo hivyo, chama cha mpira wa miguu wilaya ya Mbozi kinahitaji msaada wa hali na mali ili kuiwezesha timu hiyo kufanikiwa.
Timu ya Kimondo iko katika kundi inayozihusisha timu nane za Burkina Faso,Polisi na Mkamba Rangers za Morogoro,Majimaji na Mlale JKT za Songea,Lipuli ya Iringa,na Kurugenzi ya Njombe.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo ambayo imetolewa na chama cha Mpira wa miguu nchini TFF ni kwamba ligi hiyo inatarajia kuanza Septemba 14 na kukamilika Oktoba 27 ambapo timu zitacheza kwa mtindo wa ligi ya nyumbani na ugenini.













Post a Comment