Ads (728x90)


Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao anayeanza kwa kueleza kwa nini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.

Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na
mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.

Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.

Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wakotayari kumtolea mahari.

Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.

Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.

Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi wa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchaguwe mnmoja wao alishindwa akisema anawapenda wote wawili.

Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa kwenda kumjulia hali.
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
Nchini Tanzania nako mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo Sumbawanga Veronica Salehe(50)aliliripotiwa kuishi na wanaume wawili zaidi ya miaka saba kwa wakati mmoja.
Mwanamke aliishi na wanaume hao baada ya makubaliano baina yake na wanaume hao waliotambulika kwa majina ya Paulo Sabuni(60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele(45) mume mdogo.
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye alikuwa na amri kuu katika nyumba hiyo hata kufikiria kuwa yeye ndiye aliyewaona wanaume hao.
Mwanamke huyo mwenye watoto wanne wakiwemo watoto watatu wa kiume mkubwa akiwa na umri wa miaka 20 na binti mwenye umri wa miaka 16 amekuwa akiwapangia zamu ya kulala waume zake.Inadaiwa kuwa mume wa pili aliwahi kuwa na mke ambaye aliachana naye baada ya kuanza mapenzi na mkewe wa sasa.(vyanzo..BBC SWAHILI/ Habarileo)






Post a Comment