Ads (728x90)Mmoja wa waratibu wa Tanzania College Festival Joan Kiggundu akisalimiana na mkaguzi wa polisi Samora Salaga aliyemwakilisha kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya katika tamashala la Vyuo Vikuu Jijini Mbeya leo asubuhi.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Jiji la Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mwakilishi wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya

Mkurugenzi wa Highland Fm Radio Jaquline Mwakyambiki akitoa nasaha kwa wanazuoni wa Vyuo vikuu vya Jijini Mbeya walioshiriki tamasha la Vyuo Vikuu katika ukumbi wa Chuo Kikuu Mzumbe

Mmoja wa waratibu wa Tamasha la Vyuo Vikuu Joan Kiggundu akiwa karibu na keki iliyoandaliwa kwa ajili ya tamasha hilo

Burudani mbalimbali zilisindikiza tamasha hili msanii mahiri  Hafidh Malima maarufu kwa jina la Loyaloya akikonga nyoyo za mashabiki kwenye Tamasha hilo

Loya Loya akitoa burudani kwa nyimbo za kizazi kipya
Baadhi ya wanazuoni wa vyuo mbalimbali Jijini Mbeya wakiwa katika tamasha hilo
 
Mkurugenzi wa Highland Fm Radio Jacquline Mwakyambiki,mgeni rasmi mwakilishi wa RPC Samora Salaga na baadhi ya wageni wengine wakiwa wamesimama kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha hilo.


Wanazuoni wa vyuo mbalimbali Jijini Mbeya wakishangilia tukio katika tamasha hilo


Mkurugenzi wa Highland Fm Radio Jacquline Mwakyambiki akichukua kipande cha keki ambacho alikinunua kwa sh.elfu 30 kuchangia uendelezaji wa matamasha aina hiyo katika vyuo vikuu nchini.

Mwakilishi wa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Samora Salaga akitoa nasaha kwa wanazuoni wa vyuo Vikuu waliohudhuria katika tamasha hilo


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe John Steven akiendesha Quiz kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Mzumbe na MUST, Mzumbe walishinda maswali kwa Point 10 dhdi ya point 3 za MUST

Mwanafunzi wa mwaka wa 3 chuo Kikuu cha Mzumbe Nickson Barack ambaye ameandika vitabu viwili vya "Art to Heart na Kalamu ya Profesa'' akitoa ufafanuzi juu ya uandishi wa vitabu vyake

Mwandishi wa Vitabu Dishon Barack akionesha moja ya kazi zake za UandishiMkurugenzi wa Highland Fm Radio Jacquline Mwakyambiki akitoa nasaha
Washiriki wa Quiz kutoka Chuo Kikuu cha Mbeya(MUST) na Chuo Kikuu cha Mzumbe Mbeya Campus
Post a Comment