Ads (728x90)Katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye akikipitia makarabrasha ndani ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine alipokuwa akiukagua leo asubuhi, (kulia )ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala (kushoto) Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)Nicholas Musonye akikagua uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine leo asubuhi
Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye akiweka kumbukumbu katika kalabrasha lake baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa MREFA Elias Mwanjala kwenye uwanja wa Sokoine leo asubuhi
Baadhi ya waandishi wa Habari wakizungumza na Katibu Mkuu wa CECAFA katika uwanja wa Sokoine leo asubuhi
Katibu wa CECAFA Musonye akiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alipotembelea uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leoMkurugenzi wa Ufundi TFF akitoa maelekezo mbele ya Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye na waandishi wa habari leo asubuhi kwenye ofisi za chama cha Mpira wa Miguu MREFA ndani ya uwanja wa SokoineSHIRIKISHO la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesifu jitihada za timu ya soka ya  Mbeya City  kwa kubadilisha muelekeo wa ushabiki na kuiweka ramani ya soka nchini kwa kuuondoa ushabiki wa soka uliozoeleka wa kushangilia timu za Simba na Yanga.

Akizungumza Jijini Mbeya Katibu Mkuu wa (CECAFA) Nicholas Musonye alisema kuwa Tanzania ilizoeleka kwa ushabiki wa timu za Yanga na Simba, na kwamba kuibuka kwa timu za mikoani kumeleta changamoto mpya ya taswira ya kukua kwa soka nchini.
‘’Ushabiki wa Simba na Yanga naona umeanza kupungua baada ya kuibuka kwa Mbeya City, jitihada hizi tutazienzi ili kukuza kiwango cha soka katika nchi zetu za Afrika Mashariki na Kati,’’alisema Musonye ambaye pia ni mratibu wa Shirikisho la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika CAF.
Musonye ambaye alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alisema kuwa CECAFA imeichangua timu ya Mbeya City kushiriki katika michuano ya Kombe la CECAFA la nchi zinazozunguka mto Nile(CECAFA NILE CUP) ambazo zinazotarajiwa kuanza Mei 22 na kumalizika Juni 4 katika makundi manne nchini Sudan.
Musonye alitaja makundi hayo kuwa ni Khartoum ambako kutakuwa na vituo viwili vya mashindano,Port Sudan kituo kimoja na Al Shanti ambapo jumla ya timu 16 zitashiriki mashindano hayo.
Alizitaja timu hizo na nchi zake katika mabano kuwa ni El mereikh, Al Shant na El Arab(Sudan),Victoria University(Uganda)Defence(Ulinzi)(Ethiopia),Mbeya City(Tanzania  Bara)Polisi(Zanzibar) Polisi(Ruanda) Ports(Djibout) Elmas(Somalia) AFC Leopard(Kenya),Flambeau(Burundi) na Ismailia na Arab Contractors(Misri).
Katika hatua nyingine Musonye ambaye aliukagua uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine aliwataka viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kuendelea kuukarabati uwanja huo ili uweze kukidhi viwango vya michezo ya Kimataifa.
‘’Endeleeni kuumarisha uwanja wenu, nimeuona, mambo mengine yapo kiutawala nitapeleka ripoti yangu CECAFA,’’alisema bila kufafanua Musonye.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala alisema kuwa ujio wa CECAFA mkoani Mbeya unatia moyo wa kuendelea kuukarabati uwanja huo ili ikiwezekana ukubalike katika michezo ya Kimataifa.
‘’Tunashukuru kupata fursa hii naona tumeanza kuungwa mkono Kimataifa, tunaendelea kuthamini mchango wa TFF kwetu, tupo katika mikakati wa kuufanya uwanja wa Sokoine uwe ni wa Kimataifa,’’alisema Mwanjali.


Post a Comment