Ads (728x90)

Moja ya Tuzo zilizotolewa kwa shule ya Sekondari ya Wiza iliyopo Mbozi Mbeya kutokana na kufanikiwa katika BRN

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akipongeza Jitihada zilizooneshwa na shule mbalimbali mkoa wa Mbeya kwa kushika nafasi ya tatu katika Matokeo Makubwa Sasa(BRN)

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Wiza Charles Chenza akitafakari baada ya shule yake kutangazwa kuwa ni moja ya shule zilizofanya vizuri katika BRN

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi tuzo na Ngao ya Kipekee Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Wiza kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na mafanikio iliyoonesha kwa BRN

Picha ya pamoja ya viongozi wa shule ya sekondari Wiza, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Katibu Tawala Mariam Mtunguja baada ya shule ya sekondari Wiza kuwa ni shule ya kwanza mkoani Mbeya iliyofanya vizuri katika matokeo makubwa sasa BRN

Ngao ya Kipekee kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kwa shule ya Sekondari ya Wiza

Mkurugenzi wa Wiza Sekondari Charles Chenza akiwa ameshikilia ngao ya Kipekee kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kuthamini mchango wa shule hiyo kwa Matokeo Makubwa Sasa(BRN)Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Mbozi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Dkt. Michael Kadeghe baada ya kupata vyeti na tuzo ya mafanikio katika BRN

Baadhi ya wakuu wa shule na Mofisa Elimu waliohudhuria kikao

Wakuu wa wilaya (kutoka) kushoto Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dkt.Michael Kadeghe, Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kifu na Mkuu wa wilaya ya Momba Abihudi Saideya wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakati wa utoaji tuzo na vyeti kwa shule zilizofanikiwa katika Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Post a Comment