Ads (728x90)

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika mtaa wa Itiji.
Askari polisi nao walivinjari maeneo ya mkutano wa chama hicho hali ambayo ilisababisha viongozi wa CHADEMA kulijia juu jeshi la Polisi wakidai kuwa jeshi hilo linafanya kazi kwa shinikizo la kisiasa.
 

Mbunge wa Mbeya mjini Sugu akiwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA alipofanya mkutano wa hadhara mtaa wa Itiji ambako Mwenyekiti wa mtaa huo kwa tiketi ya CHADEMA Ezekiel King alifariki mwanzoni mwa mwezi huu akitumikia kifungo cha miaka 7 gerezani.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara mtaa wa Itiji
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo kimesema kuwa kitaendelea kumtupia lawama Meya wa Jiji la Mbeya na Diwani wa Kata ya Itiji Athanas Kapunga kwa kuwa yeye ni sababu ya chanzo cha kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa huo Ezekiel King aliyefia gerezani akitumikia kifungo cha miaka 7 kwa kosa la kujeruhi.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara, viongozi wa chama hicho walidai kuwa wanaamini moja kwa moja kuwa kifo cha kiongozi wao kimesababishwa na Meya huo kutokana na kuwepo kwa tofauti na chuki za wazi zilizooneshwa na Meya huyo alipokuwa hai.
''Tunaamini kuwa kifo cha Kamanda King kina mkono wa mtu, marehemu alikuwa kiongozi wa CCM, baadaye kwa chuki wakatofautiana na Diwani wa Kata hii, Mheshimiwa Kapunga, alimfanyia fitina hadi akakihama chama hicho na kuingia CHADEMA, aligombea uongozi wa Mtaa akashinda kwa kishondo uchaguzi kwa tiketi ya CHADEMA,kuanzia hapo amekuwa adui mkubwa wa Mheshimiwa Kapunga, ''alisema Mwenyekiti wa chama hicho John Mwambigija.
Mwambigija alisema kuwa kwa vyovyote itakavyokuwa iwe mchana au usiku liwe jua au baridi watahakikisha wanashinda uchaguzi wowote utakaofanyika katika mtaa huo hata kama zitatumika nguvu za dola kuudhibiti.
Naye Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Mbilinyi 'Sugu' alisisitiza kuwa kifo cha King kimeongeza chachu ya ushindi kwa ucaguzi wowote utakaofanyika katika Mtaa na kata hiyo na kuongeza kuwa wataelekeza nguvu kubwa katika uchaguzi wowote utakaofanyika kwenye kata hiyo ili kumuenzi kiongozi wao ambaye wanaamini kifo chake kina mkono wa mtu.

Post a Comment