Ads (728x90)

Mwanasiasa machachari na wakili wa kujitegemea Sambwee Shitambala(kulia)akiongozana na wakili anayemtetea, Tasco Luambano(katikati) na wakili mwenzao, Jackson Ngonyani wakitoka nje ya jengo la Mahakama Kuu leo asubuhi baada ya kuahirishwa kwa kesi ya jinai inayomkabili ya kumuudhi Singasinga.







Wakili Shitambala akijadiliana na wakili anayemtetea Luambano nje ya mahakama leo asubuhi.



Wakili Sambwee Shitambala akibadilishana mawazo na mawakili wenzie mara baada ya kuahirishwa kwa kesi inayomkabili ya kumuudhi Kalasinga


 Wakili na mwanasiasa machachari Mkoani Mbeya Sambwee Shitambala amejikuta matatani baada ya mfanyabiashara raia wa Kiasia Jaswinder Palsingh mkazi wa Jijini Mbeya kumtia  matatani  mwanasiasa huyo na kusababishwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi mfawidhi wilaya ya Mbeya.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo wakili wa serikali Ahmed Stambuli, Shitambala anadaiwa kumfanyia maudhi Singasinga huyo kwa kuingia kwa jinai na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 Kitalu BB vilivyopo eneo la Gombe Uyole jijini Mbeya ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali halali ya Kalasinga huyo.

Shitambala ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM(mnec) amedaiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni, 18 2012 na Novemba 28,2013.

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, Wakili wa Stambuli alisema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuingia kwa jinai kinyume cha sheria namba 79 ya mwaka 2014 kinyume cha kanuni namba 16 za sheria ya adhabu.

Mara baada ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa ambaye alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo hakimu Ndeuruo alisema kuwa dhamana ya mshitakiwa iko wazi na anaweza kuwa nje kwa dhamana iwapo atatimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha sh. milioni 1.

Mshitakiwa ambaye hakuwa na mdhamini aliruhusiwa kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya fedha sh. milioni 1.

Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.

Akizungumza nje ya mahakama wakili anayemtetea Shitambala, Luambano alisema kuwa mteja anawakilisha wakazi wengine 400 ambao wamejenga pamoja naye katika eneo hilo na kuwa hata hivyo ameshitakiwa yeye peke yake.

Aidha washitakiwa wengine wanne ambao walikamatwa pamoja na Shitambala na kufika mahakamani hapo hawakuhusishwa na kesi hiyo na kutakiwa kukaa pembeni kwa kuwa kesi hiyo haikuwahusu wao.

Waliokuwa pamoja na Shitambala mahakamani hapo ambao waliwekwa pembeni kwa madai kesi hiyo haiwahusu ingawa walikamatwa na polisi na kufikishwa kituo cha polisi cha Kati Jijini Mbeya, hapo ni pamoja na Jane Kamage, Hilda Ngowi,Clavery Mayangu na Said Mpunga.



Post a Comment