Ads (728x90)

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akihutubia wananchi wa kata ya Maanga leo jioni
Wakati akiendelea na mkutano gari lililobeba askari wa kutuliza ghasia wakielekea lindoni lilikatisha katika mkutano wake na kuleta taharuki  kwa wananchi
Mbunge Sugu aliwatuliza wananchi na kuwaonya askari polisi kufuata taratibu za kazi kwa kupita katika njia zilizoruhusiwa kwa kuwa kufanya hivyo kunawajengea hofu wananchi wanaohitaji kusikiliza utekelezaji wa sera na ilani za chama chao.
Sugu alitumia fursa hiyo ya kuzungumza na wananchi kuwasomea matumizi za miradi za mfuko wa Jimbo kiasi cha Sh. milioni 93 zilivyotumika kwa miradi mbalimbali ya Jiji la Mbeya.
  
Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jiji la Mbeya Baraka Mwakyabula akizungumza kabla ya kuwakaribisha viongozi jukwaani.

Naye Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Mbarali Jidawaya Jidawaya akielekezea mikakati ya kukiimarisha chama na kukijenga chama hicho na hatimaye kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015
 
Katibu Mwenezi wa Jimbo la Ubungo Jijini Dar es salaam Emmanuel Lema naye alikaribishwa na kuelezea namna ambavyo CHADEMA Jiji la Mbeya kilivyojiimarisha na kutoa matumaini ya ushindi kwa chaguzi mbalimbali zijazo za chama hicho.

Baadhi ya wananchi walioshiriki kusikiliza mkutano huo.


 
Mkufunzi wa mafunzo CHADEMA ni Msingi Nyanda za Juu Kusini Pascal Haonga akielekeza mipango madhubuti iliyofanikiwa juu ya CHADEMA NI MSINGI.
 


 
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, John Mwambigija akisisitiza uimara wa chama hicho na kudai kuwa jimbo hilo litaendelea kuwa mikononi mwa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa 2015
 
 
Baadhi ya wazee walijisogeza na mpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu kwa hotuba yake.




Taarifa za miradi ya fedha za Mfuko wa Jimbo

 

Post a Comment