Ads (728x90)

Ofisa Tawala Wilaya ya Mbeya Geofrey Annania akikabidhi bendera ya Taifa kwa viongozi wa timu ya soka ya CWT mkoa wa Mbeya ambayo inawakilsha timu za Walimu za Walimu, michuano hiyo inaanza kufanyika Agosti 18 mjini Livingstone nchini Zambia.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya CWT mkoa wa Mbeya
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya SATO nchini Zambia timu ya walimu mkoa wa Mbeya wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa hafla fupi ya kuagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa jana kwenye ukumbi wa White Pub Jijini Mbeya.
Aina ya kitambulisho kwa wachezaji ambao ni wawakilishi wa michuano ya Shirikisho la Vyama Vya walimu Kusini mwa nchi za Afrika (SATO) ambayo inaanza Agosti 18 nchini Zambia.
Ofisa Tawala wa wilaya ya Mbeya Geofrey Annania akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Mbeya Nelusigwe Kajuni na Katibu wa CWT mkoa Kasuku Bilago
Bendera ya TAIFA ambayo imekabidhiwa kwa wachezaji wa timu ya CWT mkoa wa Mbeya kuiwakilisha Tanzania nchini Zambia.
Nahodha wa timu ya CWT Macmussy Njegite
Kikosi cha timu ya Soka CWT wakiwa na viongozi






KIKOSI cha timu ya soka ya Chama Cha Walimu (CWT)mkoa wa Mbeya chenye jumla ya wachezaji 14 na viongozi wanne kinawakilisha Watanzania kwenye michezo ya Shirikisho la Walimu Kusini mwa Afrika(South African Teachers Organization(SATO) yatakayoanza Agosti 18 mjini Livingstone nchini Zambia.
Kikosi hicho ambacho kinaongozwa na Rais wa (CWT) Gratian Mukoba kinatarajia kukutana na nguli wa soka katika nchi za Kusini mwa Afrika ambazo ni pamoja na Malawi, Zambia,Namibia, Botswana,Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini.
Akizungumza michuano hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji hao Jijini Mbeya Katibu wa CWT mkoa wa Mbeya Kasuku Bilago alisema kuwa mkoa wa Mbeya umepata heshima kubwa kuwawakilisha Walimu wa  Tanzania katika michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 18.
Alisema michezo hiyo inashirikisha Vyama vya Walimu Kusini Mwa nchi za Afrika ambazo ni mwanachama wa Shirikisho linalowaunganisha  walimu katika nchi hizo(SATO) ambapo michezo hiyo itachezwa kusini mwa nchi ya Zambia katika mji wa Livingstone.
Kwa upande wake Kocha mkuu wa timu hiyo ya walimu  Ibrahim Ahaz Kasegese alisema kuwa wachezaji wako katika maandalizi mazuri ya ushindi  ambapo kwa muda wote walikuwa katika maandalizi ya ya Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara (SHIMIWI).
Alisema kuwa anajivunia kuwa na kikosi imara ambacho anaamini kitawajengea heshima walimu na Watanzania ambapo wachezaji wote wa timu hiyo ambao ni walimu mbalimbali wa shule za msingi na sekondari wana ari kubwa ya kushinda na kurejea wakiwa kifua mbele kwa kutwaa kombe.
Akizungumza kwa niaba ya serikali wakati akikabidhi bendera ya Taifa kwa timu hiyo Ofisa Tawala wa wilaya ya Mbeya Geofrey Annania alisema kuwa mbali na kushiriki michuano hiyo na matumaini ya ushindi, washiriki hao wanapaswa kuutangaza mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.
Alisema michezo hiyo itaimarisha na kuongeza undugu na ujirani mwema baina ya nchi washiriki na kuwa fursa hiyo itumike kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma katika masuala ya elimu na kuongeza chachu ya mafanikio kwa kuambukizwa na nchi zilizopiga hatua kielimu kati ya nchi hizo.
‘’Tumieni fursa hii kujifunza na kubadilishana uzoefu kitaaluma ili tuongeze weledi katika ufundishaji mashuleni,’’alisema Annania.
Kadhalika alishauri CWT ijiwekee mikakati ya kuunda timu ya kudumu ambayo hatimaye itapata fursa ya kushiriki michuano ya ligi mbalimbali na baadaye kushiriki ligi kuu kama zilivyo timu nyingine zinazocheza ligi ya Vodacom.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Josia Kasasi, Bahati Mgaya,Bakari Antony,Narsis Maseta, Diwadha Mrabyo,Nicholas  Kelion,Bahati Mwakinga na Philipo Owden.
Wengine ni pamoja na Salum Zacharia,Macmussy Njegite ambaye ndiye Kapteni wa timu hiyo,Mwashilindi Mwanifumu,Wycleff Komba, Abdul Mpulinga na Yotham Ngailo.
Viongozi wanaoungana na Rais Mukoba katika msafara wa timu hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Mbeya, Nelusigwe Kajuni,Katibu wa CWT mkoa, Bilago,Mwenyekiti wa CWT Jiji la Mbeya Magdani Sindika na Katibu wake Felix Mnyanyi.

Post a Comment