Ads (728x90)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akijaribu moja ya mashine kati ya mashine 40 za kufyatulia tofali zilizotolewa msaada na Shirika la Nyumba Tanzania kwa ajili ya vikundi vya vijana  kutoka halmashauri 10 za mkoa wa Mbeya, (kulia) Meneja wa Mkoa wa NHC Antony Komba.Mkuu wa Mkoa wa MBEYA Abbas KANDORO akiweka saini kitabu cha wageni kabla ya kukabidhiwa mashine 40 za kufyatulia tofali na NHCBaadhi ya wafanyakazi wa NHC mkoa wa Mbeya

Meneja SHRIKA la nyumba mkoa wa Mbeya Antony Komba akisoma taarifa kabla ya kukabidhi mashine 40 za kufyatulia tofali kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas KANDORO.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiusifu uongozi wa Shirika la Nyumba kwa kusaidia ujenzi wa nyumba bora kwa Watanzania.

 

 

 

MKUU wa mkoa wa  Mbeya Abbas kandoro amesifu jitihada za Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) katika kuboresha makazi  na kujenga nyumba bora zinazokidhi viwango na mahitaji  ya wapangaji wake.
Kandoro alisema hayo wakati akipokea msaada wa mashine 40 za kufyatulia tofali zenye thamani  ya sh. Milioni 18 kwa ajili ya vikundi vya vijana kutoka halmashauri 10 za mkoa wa Mbeya.
‘’Mnafanya kazi kubwa kuhakikisha wakazi wanapata nyumba bora,Shirika lenu linafanya vizuri sana, mnastahili pongezi,’’alisema Kandoro.
Alisema kuwa awali Shirika hilo lilianza kukatisha tama katika utendaji wake lakini kwa kipindi cha miaka ya karibuni kimejitahidi kurejesha imani kwa wananchi na wapangaji wake kwa kuimarisha utendaji na mahusiano na jamii.
Alisema msaada wa mashine za kufyatulia tofali kwa vikundi vya vijana vimeongeza chachu ya mahitaji ya nyumba bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana.
‘’Tunahitaji kupata nyumba bora kwa gharama nafuu, kwa mashine hizi vijana watamudu kufyatua tofali imara zitakazojengewa nyumba bora,jambo hili litawakusanya vijana pamoja na kuacha vitendo viovu,’’alisema Kandoro.
Awali akikabidhi mashine hizo Meneja (NHC)mkoa wa Mbeya Antony Komba alisema kuwa mashine hizo ni kati ya mashine nyingi zilizotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kutokana na kuwepo kwa makazi duni ya walio wengi nchini.
Alisema Shirika limeguswa na hali hiyo na hivyo kuamua kuwawezesha vijana  ili waweze kutengeneza matofali ambayo watawauzia wananchi kwa gharama nafuu ili hatimaye wananchi wengi wamudu kuwa na nyumba bora kwa gharama nafuu.
Alisema shirika la Nyumba liliziomba halmashauri kuunda vikundi kwa akila halmashauri iwe na vikundi  vinne  vyenye jumla ya watu kumi ambavyo vtachagua viongozi na kufungua akaunti ya kikundi na baadaye watapatiwa mafunzo.
Komba alisema mbali na kutoa mafunzo Shirika litatoa mchango wa sh. 500, 000 kwa kila kikundi ikiwa ni mtaji wa kuanzia shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kama vile saruji.
Alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Chunya,Mbeya, Kyela, Rungwe, Ileje, Mbarali,Mbozi,Mbeya mjini,Momba na Busokelo.

Post a Comment