Ads (728x90)

Dkt.Rajab Rutengwe Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Shamba DARASA katika maonesho ya Kilimo Nane Nane
Shamba Darasa kwenye maonesho ya Kilimo Nane nane


 MKUU wa Mkoa wa Katavi Dkt.Rajabu Rutengwe ameshauri teknolojia ya habari na Mawasiliano ifike vijijini ili iwawezeshe wakulima kwenda na wakati katika kutathmini bidhaa zao za kilimo.
Dkt.Rutengwe alisema hayo wakati wa majumuisho ya kwenye maonesho ya Kilimo Nane Nane katika ukumbi wa Banda la Mifugo leo mchana.
Alisema bidhaa zinazooneshwa na wakulima zikitangazwa zitajulikana kimataifa nakuwa  ni muhimu kwa kila Halmashauri kujianzishia tovuti na Blogu ili ziendane na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Dkt.Rutengwe alisema kuwa  kilimo cha kisasa kinapaswa kwenda na wakati uliopo ambao wananchi wanahitaji kupata taarifa za bei za mazao na masoko kutoka maeneo mbalimbali nchini.
‘’Halmashauri zitangaze mambo yao katika mitandao ya kijamii, magazeti na Runinga ili taarifa zao za utendaji zifahamike vyema kwa wananchi’’, alisema.
Aidha  Dkt.Rutengwe aliwataka wakulima kutumia pembejeo na kuachana na dhana ya ardhi kutokubali mbolea na kuwa dhana hizo ni potofu ambazo zinasababisha wakulima kuzalisha chini ya matarajio ya kila mwaka.
‘’Tungeweza kufanya vizuri tungetumia mbolea na mbegu bora,ni muhimu mabadiliko ya kilimo yaendane na kasi ya kilimo bora kinachotokana na uzalishaji wenye tija,’’alisema.

Post a Comment