Ads (728x90)

Mahindi ni zao Kuu la Chakula kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambalo likilimwa kwa kuzingatia mbegu bora na mbolea linaweza kumsaidia mkulima akazalsha kwa tija.
Shamba Darasa
Shamba darasa katika banda la TAHA

Banda la maonesho ya mazao ya mbogamboga na maua la TAHA

Baadhi ya wadau wa kilimo wakiwa katika Banda la MAONESHO la Mbozi


Baadhi ya bidhaa za mazao ya Kilimo na biashara katika banda la Halmashauri ya Mbozi

Mwakibete Kasilati Meneja Uwanja wa Maonesho ya Kilimo Nane Nane akifafanua jambo kwenye majumuisho ya siku ya tano ya maonesho ya Kilimo


Dkt. Fumbuka Mwakilembe Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti Mifugo (TALIRI UYOLE)


Zao la mahindni ni moja ya bidhaa za chakula zinazozalishwa katika mikoaa ya Nyanda za Juu Kusini


Respich Maengo Kaimu Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Rukwa,


Maonesho ya Kilimo Nane Nane leo yamefikia siku yake ya  nne  tangu kuzinduliwa kwake Agosti 2 naWaziri Mkuu Mizengo Pinda huku kukiwa bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakuta wakulima mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Mikoa sita ya Nyanda za Juu Kusini ndiyo mwenyeji wa maonesho haya huku Mkoa wa Mbeya ukiwa ndio msimamizi mkuu wa Uwanja wa maonesho hayo kwa zaidi ya miaka 22.
Mbali na maudhui halisi ya maonesho hayo kuwa ni kwa ajili ya shamba darasa kwa wakulima, maonesho hayo yameleta mvuto kwa wafanyabiashara mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane mwaka huu inasema ‘’Matokeo Makubwa Sasa Kilimo Ni Biashara, inakwenda sanjari nan uhalisi wa namna ambavyo shughuli mbalimbali za Kilimo zilivyotekwa na wafanya biashara kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Rukwa Respich Maengo alikuwa ni mgeni rasmi kwa siku ya leo ambaye alitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho, wakati wa majumuisho alitoa changamoto zake na kusema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya waoneshaji hawajui dhana ya Kilimo na maonesho hayo.
‘’Nimepita kwenye mabanda mengi, lakini ajabu waoneshaji hawajui hata kauli mbiu ya mwaka huu ya maonesho haya inasemaje,?
Maengo kama walivyo wadau wengine wa Kilimo wanayo dhana hiyo kuwa maonesho hayo yameteka nyara na wafanyabiashara ambao si wakulima, changamoto kwa waandaaji wa maonesho hayo TASO kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuhakikisha kuwa maonesho haya yanakuwa ni ya Kilimo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI UYOLE) Dkt Fumbuka Mwakilembe anasema kuwa dhana hii ya maonesho inaweza kutoweka iwapo shughuli za biashara zitapewa kipaumbele badala ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambao ndio walengwa wa maonesho haya.
 Dkt. Mwakilembe anabainisha kuwa katika baadhi ya nchi shughuli za maonesho ya Kilimo haziingiliwi na maonesho mengine na kuwa ni vyema taasisi inayosimamia maonesho hayo ikaweka utaratibu wa waoneshaji halisi wa mambo ya Kilimo.
Mwakibete Kasilati ni Meneja wa Uwanja wa Nane Nane anasema kuwa changamoto hizo ni muhimu bali utaratibu wa waoneshaji wengine wasio wakulima kufanya shughuli zao katika maonesho hayo imekuwepo kulingana na mahitaji ya wananchi wanaotembelea mabanda ya maonesho.
Anasema kuwa hata hivyo changamoto hizo ni muhimu kwani zinaibua dhana mpya ya uhalisi na uwepo wa maonesho hayo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu baina ya mkulima mmoja na mkulima mwingine kutoka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Post a Comment