Ads (728x90)

Never Mwambinga(38) mwanamke pekee anayeendesha mashine kubwa za mgodini akiwa katika mashine aina ya Damper Heavy Duty 40 tones ambalo hubeba vifusi na mawe mgodini.

Never Mwambinga akiwa amekalia usukani wa mashine aina ya Damper Heavy Duty tayari kwa kuingia mgodini.

Never akijiandaa kuondoa mashine jubwa aina ya Damper Heavy Duty tani 40 kuelekea mgodini

Never Mwambinga mwanamke wa kwanza mkoani Mbeya kuendesha Basi la abiria kwa umbali mrefu, aliwahi kusafiri na abiria kutokea Mbeya hadi Arusha. 
Upo Msemo maarufu unaotumiwa na baadhi ya watu kwa nia ya kuelezea namna ambavyo wanawake wanapaswa kupewa kipaumbele katika shughuli za kila siku katika jamii, msemo huo maarufu wa Mwanamke akiwezeshwa anaweza, unapingwa na Dereva mnwanamke pekee wa Mkoani Mbeya ambaye kwa sasa anapiga mashine kubwa za mgodini.

Mwanamke huyo Never Mwambinga anasema kuwa msemo huo wa 'Mwanamke akiwezeshwa, Anaweza! umepitwa na wakati bali anasema Mwanamke anaweza kujiwezesha mwenyewe na kuweza bila kutegemea nguvu yoyote kutoka kwa mtu wa jinsi nyingine.

Never mama wa mtoto mmoja wa kike anasema kuwa jitihda zake binafsi za bidii ya kazi na kujituma ndivyo vilivyomfanya amudu kufanya kazi za kiume bila kutegemea jinsi nyingine na kuwa upo uwezekano mkubwa kwa wanawake wa aina yake kufanya mambo makubwa zaidi yake iwapo tu wanawake hao watajituma kwa kutokata tamaa kwa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa kazini.

''Bidii yangu ndiyo imenifikisha hapa, nilijitahidi kwa kila hali kufanya kazi zinazofanywa na wanaume, nami nimeweza, namudu kazi za kiume na hata nyingine kuwazidi wanaume, natoa wito kwa wanawake kutojibweteka wafanya kazi zote bila kujali kuwa kazi hizo zinawafaa wanaume pekee''anasema Never.

Post a Comment