Ads (728x90)

Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Innocent Mungy akisisitiza jambo katika kikao cha wahariri, waandaaji wa vipindi vya Redio kwenye mkutano na kamati ya Maudhui ya mamlaka ya Mawasiliano nchini ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa Dkt. Shein Jijini Mbeya.
Naibu Mkurugenzi Idara ya Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Frederick Ntobi akionesha mfano wa  gazeti linalochapichwa kwa wiki na kuelekezea umuhimu wa vyanzo vya habari katika kuipasha jamii, wakati wa mafunzo kwa Wahariri, waandaji wa vipindi vya Redio mikoa ya nyanda za juu kusini katika Ukumbi wa Dkt. Shein jijini Mbeya.
Mmoja wa waandaaji wa Vipindi vya burudani kutoka Redio ya Ibony Fm ya Iringa, Anselm Ngaiza, (Soggy Doggy)akielezea changamoto za kihabari katika sekta ya Utangazaji kwa vyombo vinavyomilikiwa na watu binafsi nchini.
Baadhi ywa watangazaji na waandaaji wa vipindi vya Redio kutoka mikoa ya Nyanda za Juu kusini wakifuatili kwa makini mafunzo kutoka kwa Kamati ya Maudhui ya  TCRA wakati wa mafunzo kwa watangazaji, wahariri na waandaaji wa vipindi kwa Redio.
Wanahabari wakijadiliana jambo na viongozi wa kamati ya Maudhui ya TCRA katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. Margareth Munyagi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya waandaaji wa vipindi kutoka Redio mbalimbali za nyanda za juu kusini

Pichani washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa


Baadhi ya waandishi wa hanabri kutoka vituo mbalimbali vya Redio wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na viongozi wa Kamati ya Maudhui ya TCRA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Walter Bgoya akichangia mada katika kikao kilichowahusisha wanahabari, waandaaji wa vipindi na wahariri wa Redio mbalimbali mikoa ya Nyanda za Juu kusini.

Mjumbe wa Kamati ya Maudhui na Mtangazaji mkongwe ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa RTD Mzee Abdul Ngarawa akichangia mada katika kikao kilichowahusisha wahariri, waandaaji wa vipindi vya Redio nchini.

Post a Comment